Habari na Angelica Sullusi, Mbeya.
Imeelezwa
kuwa maamuzi mengi yasiyo sahihi yanayofanywa na baadhi ya viongozi hutokana na viongozi hao
kukosa umakini na ubunifu katika kutoa maamuzi.
Akitoa
mada ya Uongozi kwa wanasemina zaidi ya 30 kutoka katika Asasi isiyokuwa ya
Kiserikali ya Taifa Kwanza Forum juzi katika ukumbi wa Bonanza uliopo eneo la
Forest ya zamani Jijini Mbeya Dkt.Steven Mwakajumilo amesema kuwa wakati
umefika kwa jamii kuelimishwa juu ya somo zima la uongozi.
Amesema
kuwa changamoto kubwa waliyonayo viongozi wengi ni ya kutokubali kukosolewa na
watu wa chini hata kama wamefanya makosa.
Aidha,Dkt.Mwakajumilo
amesema kuwa viongozi wengi hupuuzia taarifa za tafiti mbalimbali ama kutofanya
utafiti kabisa hivyo kuongoza kwa hisia zao binafsi badala ya tafiti za kisayansi ili kusaidia kutatua changamoto
mbalimbali za kijamii.
Pia
ameongeza kuwa sababu nyingine ya kutopiga hatua za kimaendeleo husababishwa na
viongozi wengi wenye dhamana kukumbatia vitendo vya rushwa na upendeleo pamoja
na kujipatia utajiri wa kutisha kwa kujihusisha na mikakati hewa isiyo na tija
kwa wananchi.
0 comments:
Post a Comment