Mtafiti kutoka TACRI Bwana Dismas Pancras, akishika mche wa zao la Kahawa ulioathirika na ugonjwa
unaoozesha mashina na mizizi unaitwa sterm and root rot unasababisha
virusi vya vimelea vya Emilea melea vinavyoangamiza kabisa mimea ya
kahawa na kuwa mikavu kabisa kama kuni.
*******
Habari na Mwandishi wetu.
Mgogoro
kati ya kampuni ya Lima na vikundi vya wakulima wa kahawa kuhusu
ununuzi wa zao hilo wilaya ya Mbeya vijijini umemalizika baada baraza la
madiwani la halmashauri kuruhusu wakulima kuuza zao hilo sehemu yoyote
wanayoitaka.
Akisoma
taarifa ya utafiti iliyofanywa hivi karibuni wilayani humo mwenyejkiti
wa kamati maalumu iliyoundwa kwa ajili ya kufuatilia mgogoro huo Msuba
Luoakisyo amesema wakulima wamekuwa wakilalamikia kushuka kwa bei ya zao
hilo, ununuzi holela pamoja na wizi wa kahawa zikiwa mashambani.
Katika
kikao hicho cha dharula madiwani waliafikiana kutoa uhuru wa soko kwa
wakulima kuuza kahawa, na kwamba msimamo wa bei ya zao hilo ibaki kuwa
chini ya wakulima wenyewe.
Akihitimisha
kikao hicho mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya na diwani wa
kata ya Andason Kabenga ametoa pongezi kwa madiwani hao kufikia muafaka
wa suala hilo ambalo limekuwa likisumbua kwa kipindi kirefu.
0 comments:
Post a Comment