Habari na Ezekiel Kamanga,Chunya.
Mkazi
wa Kijiji cha Mpona Malanfali,Kata ya Totowe,Wilaya ya Chunya Mkoani
Mbeya Mwile Hassan(23),ameuawa na wananchi wenye hasira kali baada ya
kutuhumiwa kumkata kiganja mfanyabiashara Bi.Judith Mpamba(47),mkazi wa
Kijiji cha Iwindi,Kata ya Iwindi Wilaya ya Mbeya Vijijini mkoani hapa.
Marehemu
alikamatwa usiku Juni 21 mwaka huu,akidaiwa kumkata kiganja
mfanyabiashara huyo wa ufuta aliyefika kijijini hapo akiwa na mwenzie
Bwana Helman Mwalindu(37) ambao walifika kijijini hapo kwa lengo la
kununua ufuta.
Marehemu
Mwile akiwa na mtuhumiwa mwenzake Bwana Frank Nzovu(Tembo) ambaye
alitokomea kusikojulikana na ni mwenyeji wa Kijiji cha Ikonya,Wilaya ya
Mbozi,walifika nyumbani kwa Bwana Shigela ambapo waliwachukua
wafanyabiashara hao hadi eneo la shamba walikodai kuwepo kwa ufuta.
Baada
ya kufika eneo hilo hali ilikuwa ndovyo sivyo baada ya vijana hao
kugeukia wafanyabiashara hao na kuwatishia mapanga wakidai wapewe
pesa,ambapo Bwana Mwalindu alitoa pesa taslimu shilingi 860,000 na
Bi.Mpamba alitoa shilingi 700,000 baada ya kukatwa kiganja cha mkono wa
kushoto na wahalifu kutokomea kusikojulikana.
Kufuatia
tukio hilo majeruhi walitoa taarifa katika Afisa Mtendaji wa kijiji
Bwana Bahati Mwanguku na Mwenyekiti Bwana Nestory Mwashadema,ambao nao
walitoa taarifa katika Kituo cha Polisi cha Galula na walifika eneo la
tukio na kuwa tafuta watuhumiwa bila mafanikio.
Polisi
walirudi siku ya pili kwa ajili ya kukitafuta kiganja cha mkono cha Bi
Mpamba ambapo walifanikiwa kukikuta na majeruhi kukiwakilisha kituoni
hapo na kukimbizwa katika Hospitali teule ya Ifisi May 26 mwaka huu,siku
moja baada ya tukio hilo majira ya saa sita mchana.
Kwa
upande wake Afisa Mtendaji wa kijiji hicho Bwana Mwanguku,amewataja
watuhumiwa wanaodaiwa kumkata kiganja mwanamke huyo kuwa ni pamoja na
Karim(anayedaiwa kushika kisu),Frank Nzovu(alishika panga),Shigela na
Mwile Hassan.
Watuhumiwa
hao baada ya kutoroka ndipo wananchi walianza msako mkali na kufanikiwa
kumkamata Shigela na Mwile Hassan,ambaye alikamatwa Juni 21 mwaka huu
usiku akiwa amejificha kichakani baada ya kutoroka kwa baba yake Bwana
Hassan Mwahasanga(60) kilometa 8 kutoka eneo la tukio kijiji cha
Masalamba,Chunya.
Katika
mapambano wananchi wenye hasira kali walimkamata mtuhumiwa hadi Ofisi
ya kijiji na baada ya kupishana na Afisa Mtendaji wa kijiji,waliamua
kuchukua matita ya ufuta na petroli ndipo walipoamua kuwasha moto na
kumteketeza mtuhumiwa ambapo kifua ba kichwa ndivyo vilisalia.
Polisi
walifika eneo la tukio saa moja baada ya tukio kufanyika majira ya saa 5
asubuhi na kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu na mara baada ya
kukamilika ndugu wa marehemu walikabidhiwa kwa ajili ya masomo.
Baba wa mtuhumiwa Bwna Hassan Mwahasanga,amethibitisha kuwa mwanae ndiye aliyeuawa ingawa ameeleza kuwa hajui chanzo cha tukio.
Aidha
wananchi wa kijiji hicho,ambao hawakupenda majina yao kutajwa,wamesema
wamechoshwa na tabia za vijana wa hao kijijini hapo na wao wameamua
kufanya hivyo ili iwe onyo kwa vijana wengine kujihusisha na vitendo vya
uporaji.
Mazishi ya marehemu yamefanyika katika Kijiji cha Totowe Juni 22 mwaka huu.
Wimbi
la nwananchi kujichukulia sheria mkononi limekithiri ingawa lawama
hutupiwa Polisi na mahakama kwa kuwaachia huru watuhumiwa na wanachi
wamekuwa hawapo tayari kutoa ushahidi hivyo mahakama huwaachia huru kwa
kukosa ushahidi.
0 comments:
Post a Comment