Chama
cha soka cha England, FA, kimetozwa faini ya Euro 5,000 (sawa na pauni
4000), kutokana na utovu wa nidhamu wa mashabiki wake ambao Ijumaa
iliyopita walijaribu kuuvamia uwanja baada ya Engldan kuishinda
Sweden.
Faini
hiyo ni kufuatia mashabiki kujaribu kuingia uwanjani baada ya England
kuishinda Sweden 3-2 katika mechi ya kundi D mjini Kiev.
Chama
cha FA kimeamua hakitakata rufaa kuhusiana na faini hiyo, na kwa kuwa
UEFA haijaitoza FA pesa nyingi, inaashiria kwamba shirikisho hilo la
soka ya Ulaya linalichukua tukio hilo kama jambo dogo.
"Tunakubali hatua iliyochukuliwa, na tunalifikiria tukio hili kama jambo ambalo limetatuliwa," taarifa ya FA ilielezea.
Baada
ya magoli ya England yaliyotiwa wavuni na Theo Walcott na Danny
Welbeck, mashabiki kati ya 20 hadi 30 walivikaribia vizuizi uwanjani,
na kutaka kuingia ndani ya uwanja wa Olympic, lakini walifanikiwa
kuifikia sehemu ya riadha tu.
Chama
cha FA, kikijitetea, kiliweza kutoa ushahidi thabiti wa video mbele ya
UEFA na kuonyesha kwamba “uvamizi” huo ulikuwa ni jambo ambalo
lilitokea ghafula, na wala mashabiki hao hawakuwa wamepanga kutekeleza
kitendo hicho.
Tukio
hilo lilichukuliwa kama jambo dogo, na hata afisa wa UEFA katika mechi
hiyo hakulitaja katika ripoti yake kuhusiana na mechi.
Chama
cha FA pia kimethibitisha kwamba hakuna mashabiki wa England
waliokamatwa aidha nchini Poland au Ukraine katika mashindano ya mwaka
huu.
Chanzo:- BBC
0 comments:
Post a Comment