Baadhi
ya dawa zilizotelekezwa na wauguzi baada ya kukiacha kituo cha
kazi,siku nne baada ya mwenge wa uhuru kukizindua kituo hicho(Picha na
Ezekiel Kamanga)..
*Dawa zakabidhiwa kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mwenyekiti wa Kijiji.
*Wanawake wawili ambao ni wajawazito wajifungulia njiani.
******
Habari na Ezekiel Kamanga,Chunya.
Wakati
Serikali ikiendelea na mchakato wa kuhakikisha huduma za kijamii
zinasogezwa jirani zaidi na makazi ya watu,Kituo cha Afya cha Kijiji cha
Mpona,Kata ya Totowe,Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya,kimeachwa bila
watumishi baada ya waliokuwa wamefikishwa kutoweka hali iliyochangia
akina mama wawili wajawazito kujifungulia njiani.
Kituo
hicho kimeachwa mikononi mwa Afisa Mtendaji wa kijiji hicho Bwana
Bahati Mwanguku na Mwenyekiti wake Bwana Nestory Mwashadewa.
Kittuo
hicho cha Afya kilizinduliwa na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru
Kitaifa Kepteni Honest Ernest Mwanossa,Mei 12 mwaka huu ambapo watumishi
wawili wa afya walipelekwa kwa ajili ya kutoa huduma ambao ni
Tabibu,msaidizi Bwana Manase Sinkamba na Muuguzi msaidizi Bi F.
Mwaisakilaambao walitipoti kituoni hapo Mei 10 na kuanza kutoa huduma
kwa wakazi wa kijiji hicho Mei 11 mwaka huu.
Aidha
kituo hicho kilifunguliwa kwa furaha kubwa kutoka kwa wananchi wakati
wa mbio za Mwenge wa uhuru,wakiamini kuwa ni ukombozi na changamoto
zilizokuwa zikiwakabili kwa sekta ya afya zimeisha.
Katika
hali ya kushangaza wahudumu hao walitoka kituoni Mei 16 mwaka huu
wakidai kuwa wao waliazimwa tu kwa muda na kwamba walipewa siku 4 za
kutoa huduma katika kijiji hicho hivyo hadi sasa kituo hicho hakifanyiwi
kazi kufuatia adha kubwa kwa wananchi zaidi ya 2000,ambao walijenga
kituo hicho kwa jitihada kubwa ambapo kiligharimu zaidi ya shilingi
milioni 4.
Wananchi
wameiomba Serikali kufanya haraka iwezekanavyo kuwaleta wahudummu
wengi,ambapo akina mama wajawazito kujifungulia njiani kutokana na
kusafiri umbali mrefu wa zaidi ya kilometa 8 kwani baadhi yao wamekuwa
wakipanda mikokoteni na wengine kutembea kwa miguu.
Hata
hivyo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Chunya amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na
kwamba si muda mrefu waganga wa kituo hicho watapelekwa kijijini humo.
Kwa
upande wake Mkuu wa wilaya hiyo Bwana Deodatus Kinawiro,amekiri kupokea
taarifa za tatizo hilo ingawa amewataka viongozi wa kijiji hicho
kuwasilisha malalamiko yao rasmi kwa barua ili aweze kuchukua hatua za
haraka kukabiliana na adha hiyo kwa wananchi.
Kituo
hicho cha afya mbali na kutoa huduma kwa wakazi wa kijiji hicho,ilikuwa
isaidie vijiji vya jirani kutokana na Jografia ya wilaya hiyo
kuzungukwa na makabila ya Maasai,Wasukuma na Wamang'ati ambao wamehamia
wakiwa na mifugo.
0 comments:
Post a Comment