Wanafunzi
wa shule ya Seminary Manow Wilayani Rungwe mkoani Mbeya usiku wa
kuamkia Juni 14 mwaka huu wamefanya uharibifu wa kuvunja mali ya shule pamoja na kuiba
vitu visivyo pungua dhamani ya shiringi milion 50.
Akiongea
na mwandishi mkuu wa shule hiyo ya Manow Watson Masiba amesema kuwa
mgomo huo ulianza mchana kwa kuwa wanafunzi hawakutaka kula Ugali bada
ya uongozi kuwaarifu kuwa siku hiyo hakutakuwa na ratiba ya wali kwa
kuwa mchele siku hiyo ulikuwa kidogo stoo,
Uongozi
wa shule ulipojitahidi kusuruhisha suala hilo kwa kaandaa chakula hicho
usiku huo lakini wanafunzi hao walianza kufanya vulugu kwa kuvunja vioo
vya majengo na kuvunja milango na kuiba kompyuta 11 za shule pamoja na
kuingia katika chumba cha kuandalia mitihani na kuchana mitihani yote
iliyo andaliwa kwa ajili ya kuanza kuifanya hapo kesho tarehe
15.06.2012.
Kwa mujibu wa maelezo ya wanafunzi na wana kijiji wanao
izunguka shule hiyo imejionyesha kuwepo kwa tofauti kati ya uongozi wa
shule na wanafunzi hivyo kufikia wanafunzi hao kutafuta sababu ya
kufanya vulugu kwa kiasi cha uharibifu wa mari za shule na kanisa.
Akiongea
na mwandishi Askofu Dr Esrael Mwakyolile amesema kuwa uharibifu ni
mkubwa sana na zaidi ya mali zisizo pungua shiringi milion 50
zimeharibiwa hivyo ameitaka serikali kupitia vyombo vya dola kuchukua
hatua kwa wale watakao bainika kuhusika na tukio hili kulipa fidia
pamoja na kuwa uongozi wa shule utawachukulia hatua za kinidham.
Naye
mkuu wa wilaya ya Rungwe Chrispin Meela kwa kushirikiana na kamati yake
ya ulinzi na usarama amekemea vikali kitendo kilicho fanywa na
wanafunzi hao ukizingatia shule hiyo ni ya Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri hivyo kuwa mfano wa tabia njema kuliko kuchukua hatua za
Kigaidi kuharibu majengo na kuiba mali za shule.
Amechumkua
hatua ya kuifunga shule hiyo hadi tarehe 02.07.2012 kwa kidato cha pili,
tatu, Nne na sita kwa kuwa imeonekana kuwa ndio viongozi wa uharibifu
huo na wanafunzi wajapo shuleni hapo waje na wazazi wao na maelezo
binafsi kwa barua.
Hadi mwandishi anaondoka hapo jeshi la polisi
liliimarisha ulinzi shuleni hapo na wanfunzi 24 wamefikishwa police kwa
mahojiano zaidi.
Na mwandishi wetu Ally kingo Rungwe
|
0 comments:
Post a Comment