Pages


Home » » MAAFISA HABARI NA VIONGOZI MKOANI MBEYA WAWEKA TABAKA KWA WAANDISHI WA HABARI.

MAAFISA HABARI NA VIONGOZI MKOANI MBEYA WAWEKA TABAKA KWA WAANDISHI WA HABARI.

Kamanga na Matukio | 05:03 | 0 comments
Habari na mwandishi wetu.
Baadhi ya Maafisa habari na viongozi Mkoani Mbeya,wamekuwa wakileta hali ya ubaguzi kwa waandishi wa habari mkoani hapa kwa kutoa mialiko kwa baadhi ya vyombo vya habari na kuwalipa pesa nyingi na wakiwemo waandishi ambao hutoka nje ya mkoa.

Hali imejitokeza mara kadhaa katika mikutano ya halmashauri mbalimbali mkoani hapa,ikiwemo Wilaya ya Mbozi na Momba kuwa kinara wa matukio hayo na kuwafanya waandishi wengine kuvunjika moyo kwa kulipwa posho ndogo hali mwandishi huyo akilipwa maelfu ya pesa wakati chombo anachofanyia kazi kina mwakilishi mkoani hapa.

Matukio ya hivi karibuni yametokea katika wilaya ya Mbozi ambapo vyombo mbalimbali vilihudhuria Baraza la Madiwani la halmashauri hiyo na kumwita mwandishi wa habari kutoka nje ya mkoa,licha ya kuwepo kwa wanahabari lukuki mkoani hapa wenye uwezo kama wake.

Katika mkutano huo baadhi ya waandishi wa habari walikosa nauli hali iliyolazimu Mwenyekiti wa halmashauri wa wilaya hizo, Bwana Erick Ambakisye kutoa nauli mfukoni mwake.

Aidha,tukio jingine limejitokeza Juni 16 mwaka huu,wilayani Momba ambapo mwandishi aliyeletwa kutoka nje ya mkoa na kutowathamini waandishi wengine waliofika,katika uzinduzi wa wilaya mpya ya Momba kushindwa kutoa posho.

Hata hivyo kwa mtazamo huo waandishi wa habari wamemtaka Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoani hapa,kuingilia kati sakata hilo,kwani lanaweza kuleta sura mbaya  na itakayosababisha waandishi wa habari,kuchukiana bila sababu za kimsingi.

Haikuishia hapo baadhi ya waandishi wa habari kutoka chombo kimoja wamekuwa wakijitokeza zaidii ya watatu,hali inayochangia Halmashauri kuingia hasara na matumizi mabaya ya fedha.

.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger