Habari na Bosco Nyambege,Rungwe.
Wananchi wa
kijiji cha Bumbiji kata ya Isange Mwakaleli wilayani Rungwe mkoani Mbeya
wamejikuta wakimwondoa mwenyekiti wa kijiji hicho baada ya kujihusisha na
ubatilifu wa mali za kijiji hicho.
Akizungumza
na kituo hiki afisa mtendaji wa kijiji hicho ASWILE MWALUKASYA amesema wananchi
hao wameamua kufanya hivyo kutokana na kutokuwa na imani na kiongozi huyo
kutokana na ufujaji wa fedha za kijiji kiasi cha shilingi laki tano.
Mwalukasya
ameongeza kuwa mwenyekiti huyo anagubikwa na tuhuma za uharibifu wa mali ya
kijiji kama simenti yenye thamani ya shilingi laki mbili pamoja nauuzaji wa
miti ya kijiji hicho yenye thamani ya shilingi laki tatu ambayo ilikuwa itumike
katika ujenzi wa nyumba za walimu kijijini hapo.
Wananchi wa
kijiji hicho wamemtaka mwenyekiti huyo arejeshe fedha hizo ili ujenzi wa nyumba
za walimu iweze kukamilika na kuondoa uhaba wa nyumba za walimu kijijini hapo.
Kwa upande
wake diwani wa kata ya isanga amethibitisha kutukia kwa tukio hilo na kuwasihi
wananchi hao kuwa na subira kwani sheria itachukua mkondo wake.
0 comments:
Post a Comment