Habari na Gabriel Mbwille,Mbeya.
Ofisa
mtendaji wa Kata ya Nsalaga Bwana Cyprian Matola anatuhumiwa
kuwadanganya watia saini benki na kuchukuwa shilingi milioni 2 na laki 8
za ujenzi wa sekondari ya kata kinyume cha taratibu.
Hayo
yameelezwa na Mwenyekiti Kamati teule iliyoundwa kufuatilia ujenzi wa
shule ya sekondari Uyole, Jelly Mwakipesile wakati akitoa taarifa ya
kamati kwenye kikao cha Maendeleo cha kata hiyo.
Kamati
hiyo iliundwa kutokana na kuwepo kwa taarifa, juu ya utaratibu mzima
ambao haukuwa sahihi wa utoaji wa fedha benki na kupelekea kukwama kwa
kazi hiyo ya ujenzi wa shule ya sekondari Uyole wakati fedha za ujenzi
zilikuwa zimetolewa.
Aidha
amesema fedha iliyokuwa ikichukuliwa benki na Ofisa Mtendaji Matola,
ilikuwa inatunzwa UWAMU Saccos katika akaunti ya mtu binafsi hali
iliyomfanya m,tendaji huyo awe anaizalisha fedha hiyo ya serikali kwa
manufaa yake.
Nao
wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya kata hiyo, walimtaka mtendaji Matola
arudishe fedha hizo zilizotumika kinyume na taratibu na pia taarifa
ifikishwe kwa Mkurugenzi wa jiji la Mbeya.
Jitihada
za kumtafuta Mkurugenzi wa jiji, Juma Idd kuzungumzia suala hilo
zimeshindikana kutokana na simu zake za kiganjani kutopatikana sanjari
na kuwa nje ya ofisi kikazi.
0 comments:
Post a Comment