Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Kampuni
ya Mtenda Rice Care ya Mkoani Mbeya imetoa shilingi milioni nne na laki
mbili,kwa vikundi vya wakulima wa zao la mpunga kwa lengo la kujenga
ghala katika Kata ya Msangano,Taraya ya Msangano,Wilaya ya Momba Mkoani
Mbeya.
Mkurugenzi
mtendaji wa Kampuni hiyo Bwna Geofrey Mtenda,amekabidhi msaada huo kwa
Mwenyekiti Bwana Matani Mwamlima kwa niaba ya wakulima wa kata hiyo.
Vijiji
vitakavyonufaika na ghala hilo ni pamoja na Kijiji cha
Msangano,Ntinga,Mnyuzi,Chindi na Ipata ambavyo vitatumia ghala hilo
kuhifadhia mpunga katika msimu wa mavuno kutokana na kutokuwa na ghala
la kuhifadhia zao hilo.
Akisoma
risala mbele ya Mkurugenzi huyo mwakilishi wa watumishi wanaolinda
mpunga wilayani humo,Bwana Juma Sichilima amesema wanaishukuru kampuni
hiyo kwa kuwapa pia mbegu bora,zilizotoa chachu ya ongezeko la kiwango
cha mavuno kwa mwaka huu,licha ya mvua kutonyesha vema katika msimu huu.
Kwa
upande wake mshauri wa Kampuni hiyo Bwana Emile Malinza,amesema kuwa
nia ya kampuni ya Mtenda ni kuhimiza wakulima kuwa na utaratibu wa
uuzaji wwa takabadhi ya ghalani kwani hiyo ndio njia pekee ya kumkomboa
mkulima.
Ameenda
mbali zaidi kwa kusema kuwa kampuni hiyo inanunua mpunga kwa bei nzuri
na pia kwa kutumia vipimo sahihi(mizani),kutokana na walanguzi hupima
mpunga kwa kutumia debe ambapo mkulima hupunjwa na kujikuta anakuwa
mtumwa wa wafanyabiashara.
Mkutano
huo ulijumuisha zaidi ya wakulima 30 ulifanyika Juni 18 mwaka huu
katika Ukumbi wa Mtenda Sunset uliopo Mtaa wa Soweto,Jijini Mbeya.
Hata
hivyo baada ya mkutano huo wakulima hao walitembelea kiwanda cha
kukobolea Mpunga cha Wella kilichopo eneo la Iyunga jijini humo na
wakulima kujifunza ukoboaji wa mpunga kutokana na msongamano hivyo
kupata ubora katika Soko la kitaifa na kimataifa.
0 comments:
Post a Comment