Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Ajali
za barabarani zimeendelea kuchukua sura Mkoani Mbeya,baada ya kutokea
ajali iliyoua watu 13 wiki moja iliyopita,baada ya gari aina ya Coaster
na Lori iliyotokea eneo la Iwalanje,Wilaya ya Mbeya Vijijini.
Juni
14 mwaka huu majira ya saa 12:30 asubuhi katika eneo la Iwambi(Stelah
Farm) gari aina ya Toyota Hiace yenye nambari T 247 BUF liligongana na
Lori kwa nyuma lenye nambari T 786 BBH linalimolikiwa na Kampuni ya
Malumalu ya Marmo Grabito Mines ya jijini Mbeya,kisha Hiace hiyo kugonga
Lori jingine lenye nambari T 699 BXU lililokuwa na tela nambari T 233
AFC.
Hiace
hiyo iliyokuwa kwenye mwendokasi imesababisha abiria zaidi ya 18
wakiwemo wanafunzi kadhaa wa shule za sekondari waliokuwa wakienda
mashuleni mwao kujeruhiwa,waliokuwa wakitokea Mwanjelwa kuelekea Mbalizi
nje kidogo ya jiji.
Aidha,gari
hilo la abiria limeharibika vibaya na baadhi ya abiria kujeruhiwa
vibaya na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa na ya Mkoa zilizopo
jijini Mbeya.
Miongoni
mwa abiria waliokuwa katika hali mbaya ni wanafunzi wawili ambao shule
wanayosoma na makazi yao kwa sasa hayajafahamika kutokana na kujeruhiwa
vibaya hali iliyowasababishia kuvuja damu nyingi.
Hata
hivyo abiria waliokuwemo katika Hiace hiyo waliathiriwa na pombe ya
kienyeji maarufu kwa jina la Kimpumu iliyokuwemo kwenye gari hiyo,baada
ya ndoo zilizokuwa zimetumika kubeba pombe hiyo kupasuka na kufanya gari
nzima kutapakaa,ambapo madaktari na wauguzi walikuwa katika wakati
mgumu kukabiliana na harufu ya pome hiyo.
0 comments:
Post a Comment