Baadhi
ya wakazi wa mtaa wa Mwanyanje, Kata ya Igawilo mkoani Mbeya wakiwa
na nyuso za huzuni baada ya mwananchi mmoja ambaye jina lake
halikufahamika mara moja kupigwa na kisha kuchomwa moto na mwili wake
kutelekezwa. Mtu huyo aliuwawa kwa tuhuma za wizi wa kitu ambacho mpaka
sasa hakijafahamika na muibiwa mwenyewe kuto tambulika.(Picha na
maktaba yetu).
*****
Habari na Angelica Sullusi,Mbeya.
Imeelezwa
kuwa zaidi ya watu 600 waliuawa kwa kupigwa na wananchi wenye hasira
kali walioamua kujichukulia sheria mkononi katika kipindi cha mwaka jana
pekee.
Hayo
yamesemwa na Wakili na Afisa wa ufuatiliaji wa Haki za Binadamu kutoka
katika kituo cha Haki za Binadamu (LHRC), Laetitia Ntagazwa wakati
akitoa mada kwenye mafunzo ya waangalizi wa Haki za Binadamu wa mikoa ya
Nyanda za Juu Kusini yaliyofanyika Jijini Mbeya.
Amesema
utafiti uliofanywa na LHRC umeonyesha kuwa katika kipindi cha mwaka
jana pekee watu zaidi ya 600 wameuawa kwa kupigwa na wananchi, hali
ambayo inaashiria kuwa vitendo vya watu kujichukulia sheria mkononi
vinazidi kukithiri nchini.
Aidha,
Ntagazwa amesema kufuatia kuongezeka kwa vitendo hivyo ambavyo ni
kinyume cha sheria za nchi na ukiukwaji wa haki za Binadamu, Kituo cha
Haki za Binadamu kimeamua kuchukua hatua ya kushirikiana na Jeshi la
Polisi kutoa elimu kwa wananchi juu ya athari za kujichukulia sheria
mkononi.
Amesema
miongoni mwa mambo ambayo LHRC kinataka kushirikiana kwa karibu na
Jeshi la Polisi ni kampeni ya utii bila Shuruti, ambapo wameamua
kuwashirikisha Polisi kila mahali wanapokwenda kutoa mafunzo ya
kuwajengea uwezo waangalizi wa haki za binadamu.
0 comments:
Post a Comment