Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali,Mkoani Mbeya Bwana Kened Ndimbo.
******
Habari na Joachim Nyambo, Mbarali.
Wakazi 18,333 Wilayani Mbarali mkoani Mbeya hawajui
kusoma,kuandika na kuhesabu hali inayozua changamoto kwa serikali na wadau
wengine kuwabadilisha wakazi hao ili watambue umuhimu wa elimu kwa watoto wao.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa halmashauri
ya wilaya hiyo Kened Ndingo uwepo wa idadi kubwa ya wananchi wasiojua
kusoma,kuandika na kuhesabu unachangia kuwepo kwa uelewa duni juu ya umuhimu wa
elimu wilayani humo
Ndingo ameyasema hayo katika kikao cha wadau wa elimu kilichofanyika
katika ukumbi wa kanisa la Lutherani katika mji mdogo wa Rujewa na kufafanua
kuwa pamoja na juhudi kubwa inayofanywa na serikali kuhakikisha kila mtoto
aanapata elimu stahili,uthamani wa elimu kwa wakazi wa wilaya hiyo unaonekana
kushuka siku hadi siku.
Amesema tofauti na maeneo mengine ambako
wakazi wanakimbilia elimu kwa kuhakikisha waanawawezesha watoto wao
kuipata,wakazi wilayani kwake hawaoni umuhimu huo na imefika waakati sasa
hawajali elimu hata kwa watoto wao.
Kwa upande wake ofisa elimu shule za
msingi Wilayani humo Rustika Turuka amesema Wilaya imekuwa ikishika kati ya
nafasi ya 6 na 8 ya ufaulu kimkoa kati ya wilaya 8 zilizopo mkoani Mbeya katika
matokeo ya darasa la saba.
Naye mmoja wa wadau waliohudhuria kikao
hicho Ophia Nzobonaliba amesema tatizo kubwa
lipo kwa jamii za wafugaji ambao wamekluwa wakiona bora watoe fidia kwa
kutopeleka watoto wao shule na kuwaacha waendelee kuchunga mifugo yao.
0 comments:
Post a Comment