Mwenyekiti
wa Muungano wa Jamii Tanzania(MJATA) Chifu Soja Masoko,akizungumza na
wananchi wa Kijiji cha Malamba,Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya,ambapo
amewaonya kutojichukulia sheria mikononi dhidi ya watu wanaodhaniwa kuwa
ni wahalifu au kwa mtu yeyote mhalifu.
Wananchi wa Kijiji hicho.
Bwana Simon Mbogo Mwatia ambaye ni mtoto wa marehemu aliyezikwa akiwa hai Rozina Mwadala(60),akiwa na Chifu Lyoto kijijini hapo.
Habari na Ezekiel Kamanga,Mbarali.
Mwenyekiti
wa Muungano wa Jamii Tanzania(MJATA) Chifu Soja Masoko,amewaonya
wananchi wa Kijiji cha Malamba,Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya kuaja mara
moja tabia za wananchi kujichukulia sheria mikononi.
Ameyasema
hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji hicho Juni 15
mwaka huu,kufuatia kitendo cha wananchi wa kijiji hicho kumzika mkazi
mmoja Rozina Mwadala(60) akiwa hai Juni 2 mwaka huu kwa kile
kilichodaiwa kuwa alikuwa akijihusisha na imani za kishirikina.
Chifu
Masoko amesema baada ya tukio hilo baadhi ya wananchi wamehama kijijini
hapo kukwepa mkono wa sheria kuchukua mkondo wake,ambapo pia shughuli
za kiuchumi zimezorota.
Aidha
amewataka wananchi hao kurudi kwa hatua walizozichukua sio suluhu,hivyo
warudi kijijini hapo na kukaa meza moja kujadiliana na sio kuamini
baadhi ya waganga wa jadi wanaoendekeza vitendo vya upigaji ramli ambayo
huchonganisha na kusababisha mauaji kwa wananchi wasiokuwa na hatia.
0 comments:
Post a Comment