Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Watu
wawili wameuawa kwa tuhuma za wizi wa ng'ombe mmoja mali ya Bwana
Rafael Sikanyika,Kijiji cha Malonji,Kata ya Ihanda,Wilaya ya Mbozi
Mkoani Mbeya.
Marehemu
hao wametambuliwa kwa majina ya Bonny Haonga(23) na Andovile
Mwasalvuwa(16) wote ni wakazi wa Ihanda kwa pamoja wanatuhumiwa
kuibakatika kijiji cha Malonji umbali wa kilometa 7 kutoka kijiji
walichokuwa wakiishi.
Tukio
hilo lilitokea Juni 13 mwaka huu limetokana na wananchi wenye hasira
kupata taarifa za wizi wa ng'ombe huyo ambaye thamani yake
haikufahamika,ambapo waliamua kumfuatilia na kuwakamata wezi hao eneo la
Ihanda Relini na kisha kuwapiga na kuwateketeza kwa moto.
Afisa
mtendaji wa Kata hiyo Bwana Amos Kyomo amesema alipata taarifa majira
ya saa moja asubuhi,June 13 mwaka huu na kisha kufika eneo la tukio
ambapo aliatoa taarifa Kituo cha Polisi Mbalizi ambao nao walifika na
kuuchukua miili ya marehemu hadi Hospitali ya Wilaya ya Mbozi kwa ajili
ya uchunguzi.
Aidha
mara baada ya uchunguzi kufanyika miili hiyo ilikabidhiwa kwa ndugu kwa
ajili ya mazishi yaliyofanyika katika maeneo ya Ihanda jioni ya siku
hiyo hiyo.
Hata
hivyo Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa Diwani
Athumani,amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba jeshi lake
linafanya uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.
Matukio
ya wananchi kujichukulia sheria mkononi yamekithiri kwa siku za hivi
karibuni Mkoani Mbeya,licha ya Polisi kuelimisha kupitia sera yake ya
polisi jamii na ulinzi shirikishi.
0 comments:
Post a Comment