Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Watu watatu wamefariki katika ajali za barabara ni zilizotokea katika matukio mawili Wilaya ya Mbozi na Rungwe Mkoani Mbeya.
Ajali
ya kwanza imetokea katika Kijiji cha Halungu,Wilaya ya Mbozi Juni 17
mwaka huu saa 1:45 asubuhi,ambapo lori lenye nambari T 801 BCJ aina ya
Fuso mali ya Bwana Allan Mgula,mita chache baada ya kuvuka daraja la
Halungu.
Dereva
wa gari hilo Bwana Jestad Nyondo alipojaribu kumkwepa mpanda baiskeli
iliparamia kifusi cha kokoto kilichoachwa barabrani kwa muda mrefu na
mkandarasi wa barabara ya Mlowo.
Gari
hilo lililokuwa na shehena ya mpunga na abiria 24 likitokea Kamsamba
kuelekea Mlowo wilayani humo,limesababisha vifo vya watu wawili mwanaume
na mwanamke ambapo majina yao hayajafahamika mara moja na majeruhi 20
kukimbizwa katika Hospitali ya Wilaya hiyo.
Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali hiyo.
Ajali
ya pili imetokea Kata ya Ikuti,Wilaya ya Rungwe Mkoani humo,ikihusisha
gari nambari T 349 ABN aina ya Toyota Hilux Pick Up,baada ya kushindwa
kupanda mlima wa Kinyika likiwa na abiria ambao idadi yake hakuweza
kufahamika lilirudi nyuma ndipo baadhi ya abiria walianza kuruka kutoka
katika gari hiyo.
Katika
harakati hizo mmoja kati ya abiria hao ambaye ni mwanamke aliruka na
kukanyangwa na gari kisha kupoteza maisha papo hapo na majeruhi mmoja
ambaye ni mwanaume amelazwa katika Hospitali ya Makandana wilayani humo.
Hata
hivyo Kamanda wa Polisi mkoani humo ACP Diwani Athuman amethibitisha
kutokea kwa ajali hizo na kutoa wito kwa madereva kuwa makini wawapo
barabarani na Jeshi hilo linajipanga kukabiliana na ajali za mara kwa
mara.
0 comments:
Post a Comment