Chuo
Kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU),kimepata uongozi mpya kupitia uchaguzi
mkuu uliofanyika chuoni hapo mapema mwezi huu,baada ya viongozi wa awali
kumaliza muda wake,kwa mujibu wa katiba ya chuo hicho.
Rais
Mstaafu Ambukeghe Imani amemaliza kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa
chuo hicho akishirikiana na Baraza lake la mawaziri.
Aidha,Tume
ya uchaguzi iliteuliwa kusimamia uchaguzi huo ikiongozwa na Mwenyekiti
wake Bwana Emmanuel Mkavenga,ambapo mchakato wa uchaguzi ulitangazwa
mapema mwezi uliopita na watu kadhaa walijitokeza kugombea nafasi
mbalimbali ikiwemo ya Urais,makamu urais na wabunge.
Awali
uchaguzi ulifanyika Mei 29 na matokeo kutangazwa Mei 30 mwaka
huu,ambapo Bwana Godbless George alitangazwa kuwa mshindi wa ngazi ya
Urais.
Kufuatia
ushindi huo Tume ilipokea rufaa kutoka kwa baadhi ya wagombea Rais
pamoja na makamu wake wana itikadi ya vyama hali iliyopelekea tume
kutengua matokeo hayo na kuitisha uchaguzi upya baada ya kupata maoni
kutoka kwa Uongozi wa Chuo.
Bwana
Steven Lespidius alichaguliwa baada ya kupata kura 454 na kuwashinda
Myombo Mawazo na Swebya Hongera ambao wote walipata kura 193 wakati kura
109 ziliharibika na jumla zilipingwa kura 949.
Kiti
cha Makamu Rais alichanguliwa Deus Petro na wote kuapishwa Juni 14
mwaka huu katika Ukumbi mpya wa TEKU na mwanasheria wa Wilaya ya Mbeya
Prosper Msivala ambapo aliwataka viongozi hao kuongoza wenzao kwa mujibu
wa katiba ya chuo hicho.
Kwa
upande wake Mkuu wa Chuo Profesa Tuli Kasimoto,kufanya kile
kilichowaleta chuoni hapo,badala ya kujihusisha na masuala ya siasa na
kuvionya baadhi ya vyama vya siasa kutoingilia katika chuo hicho
kupenyeza siasa kwani kwa kufanya hivyo ni kuwatenganisha wanachuo na
kwamba wao wapo kama familia moja.
Hata hivyo amemalizia kwa kusema utawala utatoa ushirikiano ili kudumisha mshikamano chuoni hapo.
0 comments:
Post a Comment