Habari na Ezekiel Kamanga,Chunya.
Mkazi
mmoja wa Kijiji cha Mbangala,Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya,Bwana Issah
Malala(32) anashikiliwa na Jeshi la Polisi baada ya kukutwa na silaha
aina ya gobole nyumbani kwake.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi mkoani humo Diwani Athuman,amesema mtuhumiwa huyo
alikamatwa majira ya saa 3:00 usiku,Juni 11 mwaka huu na kwamba alikuwa
anamiliki silaha hiyo kinyume cha sheria.
Ameongeza
kuwa mtuhumiwa bado anashikiliwa na jeshi lake na upelelezi ukikamilika
atafikishwa mahakamani ili kujibu shtaka la kumiliki silaha hiyo bila
kibali.
Pichani
ni gari lenye nambari T 491 ATR lililoharibiwa na madereva wa pikipiki maarufu kama
bodaboda,likiwa limeharibiwa vibaya kwa kuvunjwa vioo vyote Juni 9 mwaka
huu,majira ya saa nne asubuhi baada ya kumgonga dereva mwenzao Mtaa wa
Kabwe,Jijini Mbeya hapa kisha kutokomea.
Lakini
madereva bodaboda hao walimfukuzia mpaka Mtaa wa Mama John,Jijini
humo,ambapo walimpiga baada ya kukataa kutii amri ya kulipeleka gari
polisi.Hata hivyo hivi sasa Jeshi la Polisi wanawatafuta vijana wa
bodaboda wanaotuhumiwa kuharibu gari hilo.
0 comments:
Post a Comment