Habari na Tumaini Msowoya,Iringa.
Wataalamu
wa wizara ya afya na ustawi wa jamii wameishauri serikali kubuni njia
mpya ya ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini
ili kuepusha mitandano ya kingono inayoendelea kuiathiri jamii ya
wasomi ambayo inateketea kwa ugonjwa wa ukimwi kutokana na kukabiliwa na
hali ngumu ya maisha vyuoni.
Afisa
Ustawi wa Jamii wa Wizara ya Afya, Eliwanzita Mtebe amesema katika vyuo
vya elimu ya juu vilivyopo hapa nchini, idadi kubwa ya wanachuo katika
vyuo hivyo wanaambukizwa virusi vya ukimwi na kupoteza maisha ume vingi.
Mtebe
alikuwa akizungumza katika warsha ya siku moja kuhusu kampeni ya
kitaifa dhidi ya mitandao ya kingono maarufu kama ‘Tuko Wangapi’
iliyowahusisha Waandishi wa Habari wa mikoa ya Iringa,Njombe na Mbeya.
“Mitandao
ya ngono huko katika vyuo vikuu ni balaa na nyie ni mashahidi kwamba
wanapocheleweshewa mikopo hali huwa mbaya zaidi hasa tunapowaona dada
zetu wanavyojiuza kirahisi kwa sababu hawana fedha,wengine wakizidiwa
wanaiba na ndipo mitandao hii ya kingono inapo sambaza VVU na kila
wakati utaona wanachuo na walimu wao wanavyopoteza maisha,”alisema.
Alisisitiza kuwa ipo haja kwa serikali kuangalia upya njia bora za utoaji wa mikopo tofauti na ilivyo hivi sasa.
Kwa
upande wake, Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa,Bi. Getrude Mpaka
aliwataka wanandoa na watu walio katika mahusiano kwa waaminifu katika
mahusiano yao ili kupunguza mitandao ambayo imekuwa ikihatarisha afya
zao kutokana na mambuziki ya Ukimwi.
Alisema
mitandao ya kingono imekuwa ikiathiri Serikali baada ya tafiti za
Wizara ya Afya na Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS)
kuonyesha kuwa ya hali hiyo yanasababisha mifarakano katika familia na
kuziathiri kisaikolojia, kiafya, kielimu na hata kuendelea kuathiri
jamii kwa ujumla.
Awali,
Mganga Mkuu wa mkoa wa Iringa,Dk.Robert Mahimbo alisema kuwa asilimia
20.7 ya wanaume wote nchini na asilimia 3.5 ya wanawake kwa mujibu wa
TACAIDS,tafiti zinaonyesha kwamba wana mahusiano ya kingono kwa zaidi ya
watu wawili.
0 comments:
Post a Comment