Pages


Home » » MKUU WA MKOA WA MBEYA AWATAKA WUTIMISHI WALIOHUSIKA KATIKA KASHFA YA UKUSANYAJI WA FIDIA PASIPO KUTOA STAKABADHI KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA.

MKUU WA MKOA WA MBEYA AWATAKA WUTIMISHI WALIOHUSIKA KATIKA KASHFA YA UKUSANYAJI WA FIDIA PASIPO KUTOA STAKABADHI KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA.

Kamanga na Matukio | 04:53 | 0 comments
Na mwandishi wetu.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Bwana John Livingstone Mwakipesile amemwagiza Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Rungwe Bwana Noel Mahenga kuwafikisha katika vyombo vya sheria watumishi wa serikali waliohusika na kashfa ya kuwatoza faini ya shilingi 500 na kutowapa stakabadhi wananchi wanaodaiwa kutokuwa na vyoo pamoja na mazingira machafu ya nyumba zao.

Watumishi hao walichukua hatua hiyo walipokwenda kufanya operasheni ya usafi wa mazingira vikiwemo vyoo katika kata hiyo,hata hivyo badala ya kutekeleza kilichowapeleka waligeuza kama mbinu ya kujipatia fedha na mazao ya wakulima walioshindwa kulipa fedha hiyo.

Naye mmoja wa wananchi hao Philipo Mwakatumbula alisema kitendo kinachofanywa na idara hiyo ni kibaya kwani wanateseka kwa kushindwa kulipa shilingi mia tano na kunyang’anywa mazao yao ambayo wanategemea kwa chakula na kujipatia fedha.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger