Pages


Home » » WANAFUNZI WANAMCHANGO MKUBWA KATIKA BENKI YA DAMU KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI.

WANAFUNZI WANAMCHANGO MKUBWA KATIKA BENKI YA DAMU KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI.

Kamanga na Matukio | 04:50 | 0 comments
Picha hii ni kielelezo cha jinsi ya uchangiaji damu.
Na mwandishi wetu.
Uchangiaji wa damu salama mashuleni mkoani Mbeya umepungua kutokana wanafunzi wanaochanguliwa kujiunga na masomo ya sekondari kuwa na umri mdogo na hivyo walio wengi kukosa kutimiza vigezo vya uchangiaji damu ambapo kigezo mojawapo ni kuanzia umri wa miaka 18.

Akiongea na mwandishi wetu Meneja wa kitengo cha damu salama nyanda za juu kusini Daktari Lelo Bilihima amesema kuwa licha ya kampeni na juhudi zinazofanywa na kitengo hicho kuwa uhitaji wa damu unatakiwa kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na kiasi kilichopo katika hospitali nyingi.

Aidha ameongeza kuwa damu hiyo haiuzwi na kwa yeyote atakayebainika anauza damu hiyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

Ameeleza kuwa upungufu mkubwa wa damu katika Benki ya damu ya Kanda ya Nyanda za juu Kusini hutokea mara baada ya shule za sekondari kufungwa ambapo wamekua wakichangia kwa asilimia kubwa upatikanaji wa damu salama. 

Wakati huo huo akizungumzia upande wa wananchi Dkt. Baliyima Lelo amesema kuwa wachangiaji wengine wanaogopa ukubwa wa sindano hivyo kupunguza uchaangiaji wa damu na amewataka wananchi kuondokana na uvumi ulioenea kwa sasa kuwa mchangiaji akichangia mara moja atatakiwa kuchangia tena kwa zaidi ya mara na kusisitiza kuwa jukumu la kuchangia damu ni wajibu wa kila mmoja.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger