Pages


Home » » MAKAMU WA RAIS DKT BILAL KATIKA SEMINA YA KUBADILISHANA UZOEFU NA TAASISI YA MAZINGIRA YA STOCKHOLM

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL KATIKA SEMINA YA KUBADILISHANA UZOEFU NA TAASISI YA MAZINGIRA YA STOCKHOLM

Kamanga na Matukio | 04:26 | 0 comments
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mama Asha Bilal, Waziri wa Mazingira Huvisa, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Taasisi ya Mazingira ya Stockholm, John Kuylenstierna, wakati wakiwa katika semina ya kubadilishana uzoefu kati ya taasisi hiyo na Wizara ya Mazingira iliyo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais. Semina hiyo ilifanyika jana katika ofisi za taasisi hizo zilizopo Stockholm nchini Sweden.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mama Asha Bilal, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Mazingira ya Stockholm, baada ya kumalizika kwa semina ya kubadilishana uzoefu kati ya taasisi hiyo na Wizara ya Mazingira iliyo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais, iliyofanyika jana septemba 27 katika ofisi za taasisi hizo zilizopo Stockholm nchini Sweden.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mama Asha Bilal, wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Muhammed Mwinyi Mzale na baadhi ya mabalozi wa nchi mbalimbali baada ya hafla ya chakula cha mchana kilichoandaliwa na Balozi wa Tanzania, Sweden jana Septemba 27. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger