Mtoto Hassan Adam mwenye umri wa miaka 12 mkazi wa mtaa wa Itenzi. Nyumba namba IT/MW/669 kata ya Gombe jijini Mbeya amekuwa akinyanyaswa na kuchapwa mara kwamara na mama yake Bi Ashura Hassan na Baba yake Bwana Adam Jemedari na kumpelekea kupata majeraha kutokana na kushindwa kwenda Madrasa na kunyimwa chakula zaidi ya siku mbili na akiwa analala chini bila godoro na shuka chakavu kama picha inavyoelekeza.
Na hivyo kusababisha mtoto huyo kutoenda shule kwa zaidi ya siku za 7 kutokana na majeraha makali yaliyompelekea kushindwa kukaa. Ukatili huu dhidi ya watoto na haki za binadaamu.Kutokana na tukio hili mama yake mzazi ameamua kukimbilia mkoani Morogoro, eneo la Mang'ula
Mwenyekiti wa mtaa huo Bwana Januari Robert ameahidi kushughulikia suala hilo baada ya mtandao huu kubaini tukio hilo.
Majeraha haya jamani inasikitiza................ ubinadamu kazi tuwe na mioyo ya huruma wazazi.
Tizama kwa makini halafu jiulize hawa wazai wanalengo gani nafsini mwao.
Taswira ya picha hii ikionesha sebuleni kwa mtoto huyo
Hii ni nyumba ambayo wazazi wake wamekuwa wakiishi
Balozi wa mtaa huo Bi Lydia Sionike akishangaa majeraha ya mtoto Hassan
Binti huyu Bi Doto Kambanga ndiye anayemsaidia chakula mtoto Hassan.
Fredy Herbet ambaye ni Mwandishi wa habari na mtangazaji wa kituo cha Bomba FM radio kilichopo maeneo ya Block T jijini Mbeya akielekea Ofisi ya serikali ya mtaa wa Gombe kwa mwenyekiti Godfrey Kapunga.
Polisi na Haki za Binadamu okoeni maisha ya kijana huyu na watoto wengine ambao wamekuwa waki8kumbwa na wimbi la mateso.
0 comments:
Post a Comment