Pages


Home » » WAZAZI NCHI WATAKIWA KUWAJENGEA MISINGI YA KUTHAMINI ELIMU WATOTO WAO

WAZAZI NCHI WATAKIWA KUWAJENGEA MISINGI YA KUTHAMINI ELIMU WATOTO WAO

Kamanga na Matukio | 03:03 | 0 comments
 Na mwandishi wetu.
Wazazi wametakiwa kuwahimiza watoto wao kuzingatia masomo badala ya kuwaachia watoto wao kufanya mambo ya starehe ambayo yamekuwa yakiwaasababishia kufanya vibaya katika mitihani yao ya Taifa.

Rai hiyo imetolewa na Padre Bathromeo Kaniki katika mahafali ya pili ya kituo cha elimu ya kujiendeleza Juhudi ya liyofanyia katika ukumbi wa Kiwira jijini Mbeya jana.

Amesema wazazi wamekuwa wakichangia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kufanya vibaya kwenye mitihani yao kutokana na wao kuwanunulia zaidi vitu vya burudani kuliko vitabu vitakavyowawezesha watoto kujisomea.

Wakati huohuo amewataka watahiniwa kutumia elimu waliyoipata katika kuchanganua mambo yaliyomo ndani ya jamii ili waweze kuepukana na kujiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger