Na mwandishi wetu.
Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Mbeya, Dakta Mary Mwanjelwa (CCM), amesema licha ya sekta ya afya kukabiriwa na changamoto ya uhaba wa watendaji, lakini hicho hakiwezi kuwa kigezo cha watendaji waliopo kutoa lugha chafu kwa wagonjwa.
Dakta Mwanjelwa ameyasema hayo mara baada ya kutoa msaada wa magodoro 20, katika kituo cha afya cha serikali cha Ruanda , kilichopo Mwanjelwa mjini Mbeya.
Aliongeza zaidi ya asilimia 70 ya watanzania wamekuwa wakienda kutibiwa katika hospitali na vituo vya afya vya serikali tofauti na vile vya binafsi, na hilo huchangiwa na gharama katika hospitali za serikali ni ndogo ukilinganisha na zile za binafsi.
Aidha, ameutaka uongozi wa kituo cha afya Ruanda , kuyatunza vyema magodoro hayo ili yaweze kudumu kwa muda mrefu zaidi, hivyo kutumiwa na wanawake wengi wanaofikishwa hapo kwa ajili ya kulazwa.
Naye Mganga Mkuu wa halmashauri ya jiji la Mbeya, Dakta Samuel Razalo, ametoa shukrani kwa mbunge huyo kutoa msaada kwani wapo wengi wenye uwezo lakini wameshindwa kusaidia sekta ya afya kuendelea.
0 comments:
Post a Comment