Pages


Home » » MAAMBUKIZI YA UGONJWA WA KIFUA KIKUU YANATARAJIA KUPUNGUA.

MAAMBUKIZI YA UGONJWA WA KIFUA KIKUU YANATARAJIA KUPUNGUA.

Kamanga na Matukio | 05:02 | 0 comments


Maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu yanatarajiwa kupungua mkoani Mbeya kutokana na kupungua kwa maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

Kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Mbeya dakta Harun Nyagori amesema tangu kupungua kwa maambukizi ya virusi vya Ukimwi mkoani hapa idadi ya wagonjwa wa kifua kikuu imekuwa ikipungua.

Aidha ameitaka jamii kujitokeza kwa wingi katika vituo vya afya kupima kifua kikuu ili waweze kupata tiba mapema kutokana na tiba ya ugonjwa kuwepo.

Wakati huohuo amesema kuna uwezekano mkubwa wa magonjwa yatokananayo na ngono kupungua baada ya kufanyika kwa kampeni ya Tohara ambayo kwa asilimia 60 inasaidia kujikinga dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ambapo zaidi ya wanaume elfu kumi na nane wamefanyiwa Tohara mkoani Mbeya.

Wilaya zinazoongezeka kwa maambukizi ya ukimwi mkoani Mbeya ni Kyela, Mbarali, Mbozi na Chunya.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger