Pages


Home » » AUA MKEWE KWA JEMBE NAYE AUAWA

AUA MKEWE KWA JEMBE NAYE AUAWA

Kamanga na Matukio | 05:43 | 0 comments
Na Ezekiel Kamanga.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa Bwana Doto Njige alimuua mkewe kwa kumkata na jembe mara tatu kichwani usiku wa kuamkia Septemba 19 mwaka huu kwa kile kilichodaiwa ni wivu wa kimapenzi.

Mkewe aliyefahamika kwa jina la Selina Cheling(55) alikufa papo hapo baada ya kumkata na jembe ambapo wananchi wa kijiji cha Ubaruku walimkamata Doto Njige na kuanza kumshushia kipigo cha nguvu hali iliyofanya uongozi wa kijijini kuingilia kati na kumnusuru mkazi huyo.

Kumnusuru huko hakukusaidia chochote kwani akiwa njiani kupelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu alifariki dunia kutokana na kuvuja damu nyingi.

Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya limethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo Kaimu Kamanda wa Polisi Anacletus Malindisa amesema polisi inaendelea na msako wa kuwabaini waliohusika na kitendo hicho.

Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi mkoani Mbeya kutojichuklulia sheria mkononi kwani ni hatari na kunaweza kuvuruga amani ya Tanzania.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger