Pages


Home » » UBOVU WA MIUNDOMBINU, BEI KUBWA KWA PEMBEJEO ZA KILIMO YASABABISHA WAKULIWA WA ZAO LA VIAZI KUTONUFAIKA NA ZAO HILO.

UBOVU WA MIUNDOMBINU, BEI KUBWA KWA PEMBEJEO ZA KILIMO YASABABISHA WAKULIWA WA ZAO LA VIAZI KUTONUFAIKA NA ZAO HILO.

Kamanga na Matukio | 04:22 | 0 comments
Na mwandishi wetu.
Wakulima wa viazi kijiji cha Lusanje kata ya Mpombo Mwakaleli wilayani Rungwe mkoani Mbeya wamesema kupanda bei kwa pembejeo za kilimo na ubovu wa miundombinu imekuwa ikichangia wao kutonufaika na kilimo hicho.

Mmoja wa wakulima wa viazi hivyo Gilibert Mwasanteba amesema bei ya Mbolea ya kukuzia na kupandia na dawa za kuua wadudu zimepanda hali inayowafanya kutumia gharama kubwa kwa kilimo kuliko kipato kinachopatikana

Wakati huohuo ametoa ombi kwa Serikali kuongeza vocha za ruzuku kutokana na mfumo unaotumiwa sasa wa vocha moja ama mbili kutolewa kwa mkulima mmoja kutoendana na ukubwa wa shamba linalolimwa.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger