Wakazi 841 wa Kijiji cha Ikuti, Inyara na Sisitila waidai serikali fidia ya kuchukuliwa maeneo yao kupisha ujenzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia yaani MIST kilichopo Mkoani Mbeya, lakini mpaka sasa ni zaidi ya Mwaka mmoja na mienzi minne Serikali haijawalipa fidia hiyo na ikiendelea kutoa ahadi kila siku, huku baadhi yao wakiendelea kupoteza ndugu zao wanaowategemea kutokana na kusubiri kwa muda mrefu na hivyo kushindwa kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi na maendeleo.
Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa chuo hicho Prof. Joseph Msambichaka.
Katikati ni Prof Msambichaka na timu nzima ya Chuo hicho cha MIST wakitafakari malalamiko ya wananchi hao.
Mama huyu akilia kwa uchungu kutokana na baadhi ya mazao yake kuharibika na kushindwa kuwapeleka watoto shule kutokana na kutegemea zao la Kahawa na Migomba ya ndizi.
Prof Msambichaka amesema Septema 29, mwaka huu atakuwa na jibu kutoka Wizarani kuhusu malipo ya fidia za wananchi hao. Wizara husika tatueni kero za wananchi ambao wameiweka madarakani serikali.
Picha na Habari kwa ushirikiano wa Mbeya Yetu. Kamanga na Matukio, na Kamanga na Matukio.
0 comments:
Post a Comment