Pages


Home » » MADEREVA 7 WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA KWA KOSA LA KUVUNJA SHERIA

MADEREVA 7 WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA KWA KOSA LA KUVUNJA SHERIA

Kamanga na Matukio | 04:43 | 0 comments
 Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi.
Hapa ni kituo cha magari ya abiria aina ya daladala cha Kabwe kilichopo Mwanjelwa jijini Mbeya na kinadaiwa kuongoza kwa madereva na makondakta kuvunja sheria za usafirishaji wa abiria kwani wamekuwa wakijaza abiria katika magari hayo kupita kiasi.

Na mwandishi wetu.
Kutokana na kukithiri kwa ajali za barabarani Mkoani Mbeya jeshi la polisi Jeshi la polisi mkoani Mbeya linawashikilia madereva saba akiwemo Faraja Emmanuel aliyekutwa akiendesha gari la abiria, licha ya kuzuiwa na Jeshi la Polisi kuendesha aina yoyote ya gari ili kuepuka ajali.

Mratibu mwandamizi wa polisi Anaclet Malindisa amesema kuwa madereva hao wamekamatwa kwa makosa ya kutumia leseni ambazo muda wake umekwisha na kutumia leseni za kuendesha maroli badala yake huendesha magari ya abiria na baadhi yao wamefikishwa mahakamani.

Amewataja madereva waliofikishwa mahakamani kuwa ni Emmanuel Mwakiselise, Iddan Sanga, Igno Mgaya kwa makosa ya kutumia leseni zilizokwisha muda wake na Faratieli Sanga, Michael Mwangoloka wapo rumande kwa kosa hilo hilo.

Wakati huohuo Kelvin Mwakitange amekamatwa kwa kosa la kutumia leseni ya daraja E ambayo hutumika kuendesha malori badala ya magari ya abiria kama alivyofanya.

Mbali na hilo Malindisa amesema Jeshi la polisi mkoani humo limejipanga kupunguza ajali hizo kwa kuweka kanuni madhubuti zitakazowalazimu madereva na abiria kuzifuata na kuimarisha doria katika barabara kuu za jiji sambamba na kutoa elimu kwa madereva na watembea kwa miguu juu ya kanuni za barabara.

Amesema ni kujaza abiria kupita kiasi ni makosa kisheria kwani kitendo hicho huweza kusababisha ajali na kuwataka abiria kudai tiketi pindi wanaposafiri.

Kamanda Malindisa ameongeza kuwa ni haki ya abiria kudai na kurudishiwa nauli yake mara tu gari linapoharibika njiani ili aweze kuendelea na safari yake kupitia gari lingine.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger