Wanawake jijini Mbeya wameshauriwa kujishughulisha na shughuli mbalimbali zikiwemo kazi za mikono ili kujikwamua katika dimbwi la umaskini na kuwa tegemezi kwa waume zao.
Hayo yamesemwa na katibu wa idara ya wanawake kanisa la Moravian jimbo la kusini wilaya ya kyela BI.Idda Mwaiseba katika mahojiano wilayani humo.
Amesema mwanamke anaweza kukombolewa endapo yeye mwenyewe atachukua hatua za haraka kujishughulisha na kazi mbalimbali badala ya kutegemea kupewa huduma na mumewe.
Kwa upande wao baadhi ya wanawake wa kanisa hilo wamesema kuwa kupitia vikundi vya wanawake wameweza kupeana elimu ikiwa ni pamoja na kupata mikopo kutoka kwenye taasisi mbalimbali kwa urahisi zilizowawezesha kuanzisha shughuli mbalimbali za ujasiriamali.
0 comments:
Post a Comment