Pages


Home » » MBUNGE WA VITI MAALUM DK MARRY MWANJELWA ATEMBELEA WAJAWAZITO NA KUKABIDHI MISAADA YA MAGODORO

MBUNGE WA VITI MAALUM DK MARRY MWANJELWA ATEMBELEA WAJAWAZITO NA KUKABIDHI MISAADA YA MAGODORO

Kamanga na Matukio | 05:31 | 0 comments
Dr Marry Mwanjelwa akabidhi magodoro yenye thamani za zaidi ya shilingi milioni 6, kwa Hospitali ya Rufaa Meta, Kituo cha Afya Mwanjelwa jijini Mbeya na Hospitali ya wilaya ya Ileje, Mbozi na Mbeya Vijijini.
Akina Mama wakishangilia ujio wa Mtetezi wao Dk Marry Mwanjelwa ambaye ni Mbunge wa Viti maalum
Dr Marry akisalimiana na mmoja wa madaktari wa Hospitali ya Rufaa Meta.
Dr Marry akipata maelezo mafupi ya ujio wake katika Hospitali ya Meta.
Dr Marry akisalimiana na akina Mama wajawazito katika Kituo cha Afya Mwanjelwa
Dr Marry Mwanjelwa akipewa utaratibu na maelezo kutoka kwa Muuguzi mata baada ya kutembelea wodi la akina Mama Wajawazito.
Dr Marry akisalimiana na kuwafariji akina Mama wajawazito

 Dr Marry akitazama Kichanga kilichotupwa chooni na kuokolewa na wasamalia wema na mama yake Juni 30, mwaka huu katika eneo la Ilolo na mtoto huyo kwapewa jina la Zaina Joseph ambapo pia ni jina la mama yake ambaye mpaka sasa hafahamiki alipo,
Katika utoaji wa misaada hiyo ya Magodoro unaendelea kutolewa ambapo Hospitali ya Meta walikabidhiwa magodoro 60, Mwanjelwa walikabidhiwa magodoro 60, na Hospitali ya Ileje magodoro 60, Hospitali ya Mbozi magodoro 59 na Mbeya vijijini magodoro 14.

Dk Mary Mwanjelwa kwa siki ua jumapili atakuwepo katika kanisa la Moravian Ruanda jijini Mbeya ambapo atakabidhi msaada na vyombo vya kuhubiria vyenye thamani ya shilingi milioni tatu.

Ametoa wito kwa viongozi kutembelea vituo mbalimbali ndani ya jamii kwani watabaini kero za wananchi na kufanya jitihada za kuzitatua, kama alivyobaini yeye katika Kituo cha afya Inyala ambacho hakina Jokofu wala chumba cha kuhifadhia Maiti na kitanda cha kujifungulia akina mama wajawazito.


Akipokea zawadi Kaimu Mganga mkuu wa Kituo cha afya cha Inyala Bi Singolile Mwaipopo amemshukuru Dokta Mwanjelwa kwa misaada hiyo aliyoitoa kwani amepata faraja na kwamba wataanza huduma ya Upasuaji hivi karibuni kwani wameshapata chumba pamoja na vifaa vya kitaalamu ambavyo vitaondoa kero kwa wakazi wa vijiji sita wanaotegemea kupewa huduma katika kituo hicho.

Vijiji hivyo ni pamoja na Itewe, Inyala, Imezu, Mwashioma, Idunda, Iyawaya, Shwamwengo, Ihango na vijiji vingine kutoka wilayani Mbarali. 


Kwa upande wake Dr Mwanjelwa ameitaka misaada hiyo itunzwe ili iweze kudumu kwa muda mrefu ili waweze kuongeza vifaa vingine ambavo havipo, wilaya zilizonufaika na misaada hiyo ni Mbeya Mjini, Mbeya Vijijini, Mbozi na Ileje.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger