Pages


Home » » WAFANYABIASHARA MKOANI MBEYA WASHAURIWA KUWEKA BIMA

WAFANYABIASHARA MKOANI MBEYA WASHAURIWA KUWEKA BIMA

Kamanga na Matukio | 06:04 | 0 comments



Mama huyu akilia kwa uchungu akiangalia duka lake likililivyokuwa likiketea Septemba 16. mwaka huu kwa moto katika soko la Sido Mwanjelwa.
Soko lilivyokuwa likiteketea soko la Sido Mwanjelwa.
Baadi ya wafanyabiashara wa Soko dogo la Forest Mafhorofani ambalo nalo liliteketea siku ya Jumapili Septemba 18, mwaka huu
Dr Mary Mwanjelwa akihutubia wananchi wake.

Na mwandishi wetu.
Wafanyabiashara mkoa wa Mbeya wametakiwa kuwa na bima za biashara zao ili wanapopatwa na majanga waweze kufidiwa.

Wito huo umetolewa na Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Mbeya kupitia chama cha Mapinduzi Mary Mwanjelwa katika mahojiano na mwandishi wetu.

Amesema kuwa bima ya moto humsaidia mfanyabiashara kupunguza makali ya hasara aliyoipata mara baada ya kuunguliwa na bidhaa zake.

Aidha amewataka wafanyabiashara kuwa na vifaa vya kuzimishia moto kwenye maduka yao ili kurahisisha zoezi la kukabiliriana na moto pindi linapotokea.

Wakati huohuo ameiomba Serikali kuunda tume huru ya kuchunguza kwa kina chanzo cha tukio hilo ikiwa ni pamoja na kuitaka tume itakayoundwa kuhakikisha inatoa majibu ili kusaidia kuhakikisha matukio ya moto yasijirudie.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger