Pages


Home » » Askari Polisi Aliyeuwawa Kwa Kupigwa Nondo MkoanI Mbeya Aagwa..

Askari Polisi Aliyeuwawa Kwa Kupigwa Nondo MkoanI Mbeya Aagwa..

Kamanga na Matukio | 04:25 | 0 comments
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Evance Balama akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa askari Polisi PC Meshack Urasa ambaye aliuawa kwa kupigwa na nondo juzi Jijini Mbeya. Mwili wa marehemu ulisafirishwa leo kwenda nyumbani kwao Machame mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Advocate Nyombi akitoa heshma za mwisho kwa mwili wa askari Polisi PC Meshack Urasa ambaye aliuawa kwa kupigwa na nondo juzi Jijini Mbeya. Mwili wa marehemu ulisafirishwa leo kwenda nyumbani kwao Machame mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi
skari Polisi wakitoa wakitoa heshma za mwisho kwa mwili wa askari mwenzao, PC Meshack Urasa ambaye aliuawa kwa kupigwa na nondo juzi Jijini Mbeya. Mwili wa marehemu ulisafirishwa leo kwenda nyumbani kwao Machame mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi.
Picha Zote na Venance Matinya na Mtandao huu
Baadhi ya wakazi jijini Mbeya wakijadiliana kuhusu tatizo la upigaji Nondo mkoani Mbeya kushoto ni Mwenyekiti wa TTP Maendeleo Bwana Godfrey akiwa na Mchungaji Mwamalanga(katikati) na Mzee Mwambola Mwenye umri wa miaka 82.
Maafisa wa vikosi vya ulinzi na usalama mkoani Mbeya wakitoa heshima za mwisho kuuaga mwili wa askari Marehemu Meshack Urassa, upande wa kulia ni Kamanda wa uhamiaji wa mkoa wa Mbeya, akifuatiwa na Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi, anayefuata Mkuu wa wilaya ya Mbeya Bwana Evans Balama, anayefuata Kamanda wa Jeshi la magereza mkoani Mbeya na wengineo.
Baadhi ya askari wakiwa wamebeba Jeneza
Utani wa makabila uliibuka katika harakati za kuuaga Mwili wa marehemu Urassa baina ya Wachaga na wapare ambapo anaonekana Bwana Ernest Mdee akionesha pesa zenye thamani ya elfu hamsini kuwataka Wachaga kulipa Shilingi laki moja. Ambapo Wachaga walifanikiwa kutoa shilingi Laki moja na elfu nne ambazo zilisaidia mahitaji katika msiba huo.
Mke wa marehemu Urassa akishindwa kujizuia baada ya kuuaga mwili wa marehemu mumewe.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger