Pages


Home » » SERIKALI YALALAMIKIWA KUSHINDWA KUWADHIBITI WAPIGA DEBE MKOANI MBEYA

SERIKALI YALALAMIKIWA KUSHINDWA KUWADHIBITI WAPIGA DEBE MKOANI MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:31 | 0 comments
Stendi ya magari ya abiria maarufu kama Daladala.Kabwe Mwanjelwa jijini Mbeya.
+++++
Na mwandishi wetu.
Wakazi wa jiji la Mbeya wameilalamikia Serikali kwa kushindwa kuwadhibiti wapiga debe katika vituo vikubwa na vidogo vya mabasi hali inayopelekea usumbufu mkubwa kwa abiria.

Wakiongea kwa nyakati tofauti baadhi ya abiria katika vituo vya kabwe, Uyole, Stendi kuu na Sokomatola wamesema uwepo wa wapiga debe katika vituo hivyo umekuwa ikiwasababishia usumbufu mkubwa ikiwa ni pamoja na wengine kuibiwa vitu vyao wawapo safarini.

Mmoja kati ya abiria hao Bi.Hamida Jumaa amesema wapigadebe hao wamekuwa wakisababisha kero kwa abiria kutokana na kufanya kazi zao pasipo kufuata utaratibu ikiwa ni pamoja na baadhi yao kumia lugha chafu pindi unapokataa kupanda magari wanayokuelekeza.

Kwa upande wao baadhi ya wapiga debe wamesema shughuli ya kupiga debe imekuwa ikiwapatia fedha kwa ajili ya kuwatatulia matatizo ya kifamilia kama malazi, mavazi, pamoja na chakula na kwamba endapo wataondolewa kwenye vituo hivyo watakabiliwa na wakati mgumu wa kuzitunza familia zao.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger