Na mwandishi wetu.
Mamlaka ya maji safi na maji taka mkoani Mbeya imepata hasara ya shilingi milioni 35 kutokana na kuibiwa kwa vifaa vya kuunganishia mabomba ya maji ambayo yamefungwa kwenye mradi mpya unaojengwa na kampuni ya Sogea Satom kutoka nchini Ufaransa.
Akiongelea hasara hiyo Afisa habari wa mamlaka hiyo Bi Mery Sayula amesema vifaa vilivyoibiwa ni gate valves na air tubes zenye vipenyo vya milimita 75 hadi 400.
Aidha amesema kuwa hadi sasa watu wanne wamekamatwa na wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Mbeya.
Wahati huohuo ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa dhidi ya wezi wa vifaa hivyo, na kuongeza kuwqa zawadi ya shilingi 500,000/= itatolewa kwa atakayefanikisha kukamatwa kwao.
0 comments:
Post a Comment