Pages


Home » » TEKNOHAMA ITAKUWA NDOTO MAENEO YA VIJIJINI ENDAPO HAVITAPEWA KIPAUMBELE CHA NISHATI YA UMEME

TEKNOHAMA ITAKUWA NDOTO MAENEO YA VIJIJINI ENDAPO HAVITAPEWA KIPAUMBELE CHA NISHATI YA UMEME

Kamanga na Matukio | 03:02 | 0 comments
Na mwandishi wetu
Imeelezwa kuwa teknolojia ya habari mawasiliano(TEKNOHAMA) itakuwa ndoto maeneo ya vijijini iwapo nishati ya umeme haitapewa kipaumbele maeneo hayo.

Wakiongea na mwandishi wetu wadau mbalimbali wa sekta ya habari mawasiliano nchini wamesema kuwa muda mrefu wameshindwa kuwekeza vijijini kutokana na ukosefu wa nishati wa uhakika maeneo hayo.

Aidha utafiti uliofanywa na mtandao huu umebaini kuwa wakazi wengi wana uelewa mdogo wa TEKNOHAMA hali inayosababisha kutokuwa na uwezo wa kutoa na kupata habari sahihi kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

Hata hivyo wadau wa nishati ya umeme mkoani mbeya wameshauri wawekezaji kutumia umeme rahisi wa mionzi ya jua pamoja na bayogesi ili kuwawezesha wakazi wa pembezoni kupata huduma ya intaneti na mafunzo mengine ambayo huharakisha maendeleo ya milenia nchini.

Teknolojia habari mawasiliano imekuwa ni kichocheo cha maendeleo duniani na hivyo ulewa mkubwa wa teknolojia hiyo kumezidi kuleta ushindani katika soko la ajira kwa vijana.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger