Mheshimiwa Dk Mary Mwanjelwa ambaye ni Mbunge wa viti maalum mkoani Mbeya akikabidhi Vyombo vya muziki vyenye thamani ya shilingi milioni 15, kwa Kanisa la Moraviani Tanzania Jimbo la Kusin Magharibi, Ushirika wa Ruanda Jijini Mbeya. Kulia aliyevalia Joho jeupe ni Mwenyekiti wa Kanisa hilo Mchungaji Nosigwe Buya ambaye alipokea vyombo hivyo
.Bwana Mboka Mjafula aliyeinama na kulia ni Siofael George wakirusha matangazo ya moja kwa moja ya Ibada hiyo kupitia kituo cha Baraka FM Radio ambayo inamilikiwa na kanisa hilo.
Wanakwaya wakipiga vyombo walivyokabidhiwa na Dk Mwanjelwa.
Dk Mwanjelwa akiingia katika ibada.
Dk Mwanjelwa katikati akiwa na akiwa na Mwenyekiti wa soko la Sido Mwanjelwa lililoungua Bwana Charles Syonga.Maandamano yakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa kanisa la Moravian Mchungaji Zacharia Sichone, ambayo yalianzia katika nyumba ya mchungaji Kanisa la Moravian Ruanda na kuelekea Kanisani.
Hii ni kamati iliyoratibu upatikanaji wa vyombo hivyo vya muziki kutoka jijini Dar es salaam wa kwanza kushoto ni Bwana Jacob Mwasanga, anayefuatia Charles Mwakyusa(Bwana Mipango), Katibu ni huyo Binti wenye sketi ya Pink Grady Mwasalemba.
Kwaya kuu iliyokabidhiwa vyombo
Kwaya ya vijana Ruanda
Mwenyekiti wa kanisa la Moravian Mchungaji Buya akimtambulisha Dk Mwanjelwa mbele ya waumini wa kanisa hilo
Mchungaji Buya ambaye ni Mwenyekiti wa kanisa hilo akihubiria waumini Neno la MUNGU
Zoezi la uimbaji wa nyimbo kutoka kwenye vitabu ukaanza
Kwaya ya NLC kutoka Kiwila wilaya ya Tukuyu ambao walialikwa katika sherehe za uzinduzi wa vyombo hivyo.Mbunge wa viti maalumu kupitia Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Mbeya Dakta Mary Mwanjelwa amekabidhi msaada wa vyombo vya muziki vyenye thamani ya shilingi milioni 15 ambapo alichangia milioni 4 kwa wanakawaya wa kanisa la Moroviani usharika wa Ruanda Mbeya.
Dakta Mwanjelwa amesema msaada huo ameutoa ili kuiwezesha kwaya hiyo kuongeza nguvu ya kuhubiri Neno la Mungu kupitia uimbaji.
Pamoja na misaada hiyo pia Dakta Mwanjelwa ametoa misaada ya vitanda na magodoro kwa hospitali ya wilaya zilizopo mkoani hapa ili kuboresha huduma za afya hasa kwa wanawake wajawazito.
0 comments:
Post a Comment