Pages


Home » » MOTO WATEKETEZA SOKO DOGO LA FOREST MAGHOLOFANI JIJINI MBEYA

MOTO WATEKETEZA SOKO DOGO LA FOREST MAGHOLOFANI JIJINI MBEYA

Kamanga na Matukio | 10:02 | 0 comments
Moto wateketeza soko hilo lililopo Forest ya zamani karibu na Chuo cha Mzumbe na Chuo Kikuu huria Jijini Mbeya
 Moto ulianza majira ya saa 9:00 kamili usiku na Zimamoto walifika saa 9:10 na kufanikiwa kudhibiti moto huo ambao umeteketeza vibada kadhaa na kusababisha hasara kubwa.
Mtandao huu umefanikiwa kukuta baadhi ya masalia ya vibanda yakifuka moshi.
Mkuu wa wilaya Bwana Evans Balama asaidia kuzima Moto huo, lakini wadau wanajiuliza kunani katika masoko ya Mbeya na kwanini tahadhari hazichukuliwi
BAADA ya soko la Sido Mwanjelwa Jijini Mbeya kuteketea kwa moto juzi, mzimu huo wa kuteketeza masoko Jijini hapa umeendelea na kuunguza soko lingine usiku wa kuamkia leo linalojulikana kama soko la Foresti lililopo mkabala na chuo kikuu cha Mzumbe na chuo kikuu huria tawi la Mbeya limeungua moto usiku wa kuamkia jana.


Soko hilo halikuteketea lote kutokana na moto huo kuanzia eneo la barabarani ambako kuliwezesha gari ya kikosi cha zima moto cha Jiji la Mbeya kufanikiwa kuuzima kabla haujaleta madhara makubwa zaidi.


Wakizungumza na mtandao wa  www.kalulunga.blogspot.com  eneo la tukio baada ya kufanikiwa kuuzima moto huo, baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo walisema moto huo uligunduliwa na baadhi ya walinzi wa soko hilo ambao waliwaarifu wenzao wanaolinda katika chuo cha Grace kilichopo eneo hilo ambao walitoa taarifa haraka katika kikosi cha zima moto.


Walisema baada ya moto huo kuendelea kuteketeza mali zilizopo eneo hilo huku kituo cha polisi kikinusurika kuwaka moto, wananchi wanaoishi karibu na eno la soko hilo walijitokeza na kutoa msaada wa kuokoa mali hizo huku baadhi yao wakisogeza vibanda mbali na eneo la hatari.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa soko hilo Nadhil Mussa alisema anamshukuru sana Mkuu wa wilaya ya Mbeya Evance Balama kujitokeza usiku huo na kushirikiana na wananchi kuokoa mali za wafanyabiashara hao.


Aidha aliitaja idadi ya vibanda vilivyoteketea na moto huo kuwa ni tisa ambavyo ni pamoja na Maduka manne, stoo moja ya kuhifadhia mafuta ya kula na meza Nne (vichanja) vya kupangia bidhaa mbalimbali ambapo thamani yake bado haijajulikana.


Sanjari na hayo alithibitisha kuwa hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa katika ajali hiyo na kwamba pia vibaka hawakuweza kufika katika eneo hilo kwa ajili ya kupora mali tofauti na wahanga wenzao wa soko la sido Mwanjelwa ambao walikumbana na adha hizo.
Mzimu huo wa kuungua masoko mkoani Mbeya hasa katika Halmashauri ya Jiji hilo umeshindwa kujulikana ambapo vyanzo vya ajali hizo vinashindwa kutanabaishwa na Serikali.

Mkuu wa mkoa aliyestaafu Bwana John Livingstone Mwakipesile aaga akiacha matatizo makubwa ambapo anayechukua nafasi yake Bwana Abas Kandoro akikalia kiti cha moto kwa matukio ya ajali ya moto mawili mfulululizo.

Wanambeya na Watanzania tupige magoto tusali na ili Mola atupe miujiza ba misingi mipya ya kuondokana na matatizo haya.

Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger