Picha hii ni kielelezo cha miundombinu ya maji Nchini Tanzania.
Na mwandishi wetu.
Wakazi wa kijiji cha Naming’ong’o kata ya Chitete wilaya mpya ya Momba mkoani Mbeya wanalazimika kutembea umbali mrefu kutafuta maji kutokana na kijiji hicho kutokuwa na miundombinu ya maji safi
Wakiongea na nasi wananchi hao wamesema licha ya kata hiyo kuwa na mto mkubwa wa Nkana bado wanakabiliwa na tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi.
Afisa mtendaji wa kijiji hicho Venans Simkoko amesema kuwa kijiji hicho kimekuwa kikikabiliwa na tatizo la maji kwa muda mrefu na kwamba hawaoni jitihada zozote zinazochukuliwa ili kutatua tatizo hilo na kumtaka mbunge wa jimbo la Mbozi Magharibi David Ernest Silinde kulimaliza tatizo hilo kwa kipindi atakachokuwepo madarakani.
Hata hivyo huenda tatizo hilo likamaliza mapema kutokana na mpango unaoendelezwa na serikali kuwapatia huduma ya maji safi wananchi waishio vijijini.
0 comments:
Post a Comment