Pages


Home » » UPUNGUFU WA WALIMU IMETANJWA KUWA NDIO CHANZO CHA WANAFUNZI KUTOROKA SHULE

UPUNGUFU WA WALIMU IMETANJWA KUWA NDIO CHANZO CHA WANAFUNZI KUTOROKA SHULE

Kamanga na Matukio | 06:03 | 0 comments



Na mwandishi wetu.
Upungufu wa waalimu katika shule ya msingi Sinde iliyopo jijini Mbeya imetajwa kuwa chanzo cha wanafunzi wa shule hiyo kutoroka na kujiingiza kwenye makundi hatarishi.

Hayo yamesemwa na mwalimu mkuu msaidizi Bwana Kanjoka Hasimu wakati akiongea na mwandishi wetu kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo kukabiliana na tatizo la wanafunzi watoro shuleni hapo.

Amesema uchache wa waalimu umekuwa ukichangia kukwamisha zoezi la udhibiti wa wanafunzi watoro hali inayopelekea ongezeko la watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi.

Wakati huohuo amewataka wazazi kujenga ushirikiano na waalimu ili kusaidia kudhibiti vitendo vya utoro ikiwa ni pamoja na kuwaongezea wanafunzi uelewa wa masomo yao kwa njia ya wazazi kufuatilia mwenendo wa masomo ya watoto wao.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger