Pages


Home » » Msiba mkubwa na Majonzi Pemba kutokana na Ajali mbaya ya kuzama kwa mweli usiku wa kuamkia leo

Msiba mkubwa na Majonzi Pemba kutokana na Ajali mbaya ya kuzama kwa mweli usiku wa kuamkia leo

Kamanga na Matukio | 12:11 | 0 comments
Kisiwa kizima cha Pemba na Zanzibar kiujumla imetumbukia kwenye msiba mkubwa baada ya meli ambayo kiasili ni ya mizigo lakini inapakia pia abiria inayojulikana kwa jina la Spice Islanders kuzama katika eneo la bahari kuu la Nungwi nje ya kisiwa cha Unguja.
Kama Wamarekani kesho wanaomboleza matukio ya Septemba 11, Zanzibar na hasa kisiwani Pemba wanaomboleza tukio zito la Septemba 10 kwani kwa mujibu wa taarifa za kuaminika, kila familia imekumbwa na msiba huo.
Idadi hasa ya watu waliopoteza maisha yao katika ajali hiyo haijajulikana lakini kwa kawaida meli hiyo hupakia abiria kupita kiasi kiasi kwamba waliozoea kusafiria chombo hicho wanasema kuwa ukiingia katika meli hii unapaswa kuchagua mkao wa kukaa kwani mkao huo huo ndio itakaobidi ukae hadi mwisho wa safari. Kama umenyoosha miguu, kama umesimama, kama umechutama, basi inabidi ukae vivyo hivyo hadi meli itie nanga.
Wengine wanaiita meli hiyo ni ya familia kwani wanaoingia ndani huwa ni watu na wana wao na wajukuu zao.
Uwezekano wa kuwa kubwa idadi ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo ambayo kwa muda mrefu haijatokea mfano wake visiwani Zanzibar ni mkubwa hasa kwa kuzingatia kuwa hiki ni kipindi cha kuchuma karafuu ambazo thamani na umuhimu wake umeongezeka maradufu baada ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupandisha bei ya zao hilo kwa asilimia 80.
Taarifa ya serikali kupitia Naibu waziri wa Mawasiliano na Miundombinu inasema kuwa watu waliokuwemo kwenye meli hiyo ni 610, lakini watu walioshuhudia wakati meli hiyo ikipakia mizigo na abiri katika bandari za Dar es Salaam na Malindi Zanzibar wanasem kuwa idadi ya watu waliokuwemo kwenye meli hiyo ni kubwa zaidi ya hiyo iliyotangazwa na Bw. Issa Haji Ussi, Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu Zanzibar.
Kuna baada ya watu wameokolewa wakiwa hai na baadhi yao wanaendelea kuopolewa majini na taarifa zisizo rasmi zinasema kuwa maiti hao wanapelekwa Nungwi, Maisara na Mnazi Mmoja kwa ajili ya kutambuliwa na ndugu na jamaa zao na kwa maandalizi ya maziko.
Chanzo: Mzalendo net
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger