Pages


Home » » MAENDELEO YA WILAYA KIUCHUMI ,WANANCHI WA WILAYA YA RUNGWE NA VIONGOZI WA WILAYA HIYO WAPEWA PONGEZI

MAENDELEO YA WILAYA KIUCHUMI ,WANANCHI WA WILAYA YA RUNGWE NA VIONGOZI WA WILAYA HIYO WAPEWA PONGEZI

Kamanga na Matukio | 05:10 | 0 comments
Makao Makuu wa Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.
Na Mwandishi wetu.
Viongozi pamoja na wananchi wilayani Rungwe, na viongozi wa wilaya hiyo, wame.pongezwa kwa juhudi wanazozifanya katika kujiletea maendeleo, ikiwemo utekelezaji kwa vitendo sera ya Kilimo Kwanza.

Imeelezwa kumekuwa na jitihada za makusudi zinazofanyika katika ukusanyaji wa mapato ya ndani imeiwezesha halmashauri hiyo kutekeleza vyema mipango yote ya maendeleo iliyopangwa.

Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile, katika kikao maalum cha Baraza la Madiwani, kilichokutana kujadiri taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Amesema hali ya ukusanyaji wa mapato ndani ya halmashauri hiyo, ambayo imeiwezesha halmashauri kupunguza utegemezi na kuendana na malengo ya milenia 2025.

Alisema niuvyema juhidi hizo zikaendelea kuongezeka k wa halmashauri kubuni vyanzo vingine vya mapato kutokana na hali nzuri ya uchumi wa wilaya kwani bado zipo fursa ambazo zikitumika vyema zitaiwezesha halmashauri kujitegemea kwa asilia kubwa zaidi”
Amesema wilaya ya Rungwe ni sawa na mkate ulionona na inanukia fedha, lakini mapato yanayokusanywa kutokana na vyanzo vyake vya ndani bado ni kidogo kwani wanao uwezo wa kukusanya sh.bilioni 1.6 kwa mwaka.

Mwakipesile alisema kwa hali hiyo Rungwe inao uwezo wa kujitegemea kwa asilimia 6, huku asilimia kubwa ikiwa ni fedha wanazozipata kutoka serikali kuu, hali ambayo haikubaliki hata kidogo na kuongeza kwamba kwa kawaida kufanikiwa ni rahisi, lakini kuendelea kushika nafasi hiyo ya mafanikio ndiyo kazi kubwa, hivyo kumtaka Mkurugenzi mtendaji, wakuu wa idara na wafanyakazi kwa jumla, kufanya kazi kwa bidii.

Alisema suala hilo litafanikiwa kwa wao kujihusisha kikamilifu katika kusimamia sheria, kanuni na miongozo ya serikali kuhusu ukusanyaji wa mapato na matumizi ya fedha za halmashauri.

Hata hivyo Mwakipesile, alisema wilaya ya Rungwe imekuwa ya pili mkoani Mbeya kwa kupokea fedha nyingi katika mwaka wa fedha 2011/2012, kwa kupata shilingi bilioni 31.3 ikitanguliwa na wilaya ya Mbozi.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger