Pages


Home » » BEI YA MAHINDI KATIKA SOKO LA SOWETO JIJINI MBEYA YAPANDA KWA ASILIMIA 37.4

BEI YA MAHINDI KATIKA SOKO LA SOWETO JIJINI MBEYA YAPANDA KWA ASILIMIA 37.4

Kamanga na Matukio | 06:22 | 0 comments


Sokoni kumependeza leo wakati wateja wakihaha kupanda kwa bei za vyakula.
Wakazi Mbali mbali Wakiwa maeneo ya Soweto kununua mahitaji.
+++++
Na mwandishi wetu.
Bei ya mahindi kwa gunia katika soko la Soweto, jijini Mbeya imepanda kutoka shilingi elfu ishirini na mbili hadi kufikia shilingi elfu thelathini na tano.

Mmmoja wa wafanyabiashara sokoni hapo Bwana Malawa Mwinuka amesema kupanda kwa bei hiyo kunatokana na kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania na mabadiliko ya bei ya nishati ya mafuta.

Aidha amesema gunia la karanga huunzwa kwa shilingi elfu ishirini na saba wakati awali lilikuwa likiuzwa kwa shilingi elfu ishirini wakati mkungu wa ndizi huuzwa kwa shilingi elfu kumi na tano awali ulikuwa ukiuzwa shilingi elfu saba.

Naye mwenyekiti wa soko hilo Bwana Ambele Mwandalima amesema huenda bei ya mazao mbalimbali itaendelea kupanda kila siku kutokana na kupanda kwa gharama za uzalishaji na usafirishaji.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger