Pages


Home » » YANAYOENDELEA KUJIRI KATIKA NYUMBA ILIYOKUBWA NA IMANI ZA KISHIRIKINA MTAA WA MWANYANJE KATA YA IGAWILO JIJINI MBEYA

YANAYOENDELEA KUJIRI KATIKA NYUMBA ILIYOKUBWA NA IMANI ZA KISHIRIKINA MTAA WA MWANYANJE KATA YA IGAWILO JIJINI MBEYA

Kamanga na Matukio | 03:41 | 0 comments
Na mwandishi wetu.
Chama cha Machifu jijini Mbeya kimesema kuwa vitendo vya kishirikina vinavyoikabili familia ya Semeni Aroni mkazi wa kata ya Igawilo jijini hapa linaweza kumalizika endapo mmiliki wa nyumba hiyo atasema ukweli kuhusu uhalali wa umiliki wa nyumba hiyo

Akiongea na mwandishi wetu Mwenyekiti wa machifu jijini hapa Loketi Mwanshinga amesema kuwa nyumba ya Semeni Aron imekuwa ikikabiliwa na tatizo la vyombo vyake kutolewa nje na watu wasiofahamika ikiwa ni pamoja na nyumba yake kupigwa mawe.

Amesema kuwa vikombe, ndoo, masufulia na vitu vingine vya samani vimekuwa vikitolewa nje na watu wasiojulikana kwa imani za kishirikina na kwamba baada ya kufanyika kwa maombi ya kimila nyumbani hapo mawe yamesitishwa kutupwa.

Wakati huohuo Chifu Mwanshinga amesema vitendo hivyo huweza kutokea endapo mtu anaweza kufanya dhuruma.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger