Habari na mwandishi wetu.
Waalimu wa ajira mpya wa shule za msingi na Sekondari jijini Mbeya hivi karibuni wameandamana hadi Ofisi ya Mkurugenzi wa jiji, wakidai madai ya malimbikizo ya mshahara wa mwezi wa pili na watatu.
Wakiowa nje ya Ofisi hiyo waalimu hao wameyataja madai yao kuwa ni Mshahara, fedha za usafiri, fedha za kujikimu na huduma za msingi.
Aidha wameomba kuondolewa kwenye chama cha waalimu Tanzania kutokana na wao kuandikishwa uanachama na kukatwa mshahara wao pasipo ridhaa yao.
Hata hivyo mkurugenzi hukuweza kukutana nao kwa kuwa alikuwa katika kikao cha wadau wa elimu mkoani mbeya.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Mbeya Abasi Kandoro amewataka wakurugenzi wa halmashauri zote kuhakikisha wanaandaa mipango madhibuti itakayowezesha kumaliza tatizo la madai ya waalimu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kila mwajiliwa mpya analipwa stahiki zake mapema.
0 comments:
Post a Comment