Pages


Home » » WAKULIMA WAIOMBA SERIKALI KUYARUSU MAKAMPUNI YA UNUNUZI WA ZAO LA PARETO ILI KULETA USHINDANI WA BEI - MAKETE

WAKULIMA WAIOMBA SERIKALI KUYARUSU MAKAMPUNI YA UNUNUZI WA ZAO LA PARETO ILI KULETA USHINDANI WA BEI - MAKETE

Kamanga na Matukio | 04:27 | 0 comments
Habari na Angelica Sullusi, Njombe.
Wakulima Wilayani Makete Mkoani Njombe wameiomba Serikali wilayani humo kuyaruhusu makampuni mbalimbali ya ununuzi wa zao la Pareto yaliyopata vibali ili kuleta ushindani wa bei ya zao hilo kwa manufaa ya mkulima.

Wakizungumza na mwandishi wetu kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi wa Kata za Ipelele na Iniho wamesema kuwa miaka miwili iliyopita kulikuwa na mnunuzi mmoja ambaye ni Kapuni ya Pareto Tanzania(PCT) yenye makao yake makuu mjini Mafinga,mkoani Iringa.

Wamesema kuwa bei ya pareto kwa kilo moja walikuwa wakiuza kati ya shilingi 1200 hadi 1600 kabla ya kupanda bei ambapo kwa sasa wanauza shilingi 1800 kwa kilo moja katika kapuni ya PCT.

Augustino Fungo mkazi wa Kijiji cha Ipelele amesema kuwa katika msimu wa mwaka huu wamefurahishwa sana baada ya kuona kampuni nyingine imejitokeza kwenda kununua pareto katika kijiji hicho.

Amesema kuwa kampuni hiyo aliyoitaja kwa jina la KATI Enteprises Ltd. imekuwa ikimlipa mkulima shilingi 2,000 kwa kilo moja jambo ambalo hapo awali lisingewezekana kutokana na kutokuwepo kwa kampuni mshindani wa PCT ambao walikuwa wakipanga bei wanayoitaka wao kwa lengo la kujinufaisha wao na si mkulima.

Aidha,ameiomba serikali kuweka mfumo mzuri wa upatikanaji wa mbegu za pareto sambamba na pembejeo nyingine za kilimo ambazo hazimfikii mkulima kwa wakati.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kata ya Ipelele Anna Sanga amesema kuwa kuwapo kwa makampuni mengi kunasaidia kupanda kwa bei ya pareto kwa kilo ambapo alitolea mfano wa shilingi 1800 kwa kilo bei iliyokuwepo hapoa awali ambapo baada ya kampuni nyingine kujitokeza na kununua shilingi 2000 kwa kilo kumekuwa na ushindani hivyo wale wa awali kupandisha bei hadi shilingi 2050.

Ameshauri serikali kutengeneza miundombinu ya barabara ambayo hivi sasa ni chakavu sana hali inayosababisha wakulima hao kukosa soko la uhakika kutokana na barabara hizo kutopitika kwa urahisi na magari hivyo kujikuta mazao yao yakiozea mashambani ama majumbani.

Awali Mkuu wa Wilaya hiyo, Zainabu Kukwega amewaambia waandishi wa habari kuwa kampuni ya PCT imeingia mkataba na wakulima Wilayani hapo hivyo hakuna kampuni nyingine iliyoruhusiwa kununua pareto wilayani humo na wale ambao wamejaribu kufanya hivyo tayari wamekwisha andikiwa barua ya kusimamishwa kununua Pareto wilayani humo licha ya kuwa na vibali halali vya kununulia zao hilo.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger