Pages


Home » » ALIYEPOPOA GARI LA MSAFARA WA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI NCHINI TANZANIA MH. SHAMSI VUA NAHODHA APANDISHWA KIZIMBANI NA KUSOMEWA SHTAKA - MBEYA.

ALIYEPOPOA GARI LA MSAFARA WA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI NCHINI TANZANIA MH. SHAMSI VUA NAHODHA APANDISHWA KIZIMBANI NA KUSOMEWA SHTAKA - MBEYA.

Kamanga na Matukio | 03:19 | 0 comments
 
Waziri wa Mambo ya ndani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Shamsi Vuai Nahodha, akizungumza na vyombo vya habari Jijini Dar es salaam. 
*****
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mkazi wa Kijiji cha Nelo Kiloleni mji mdogo wa Tunduma Mkoani Mbeya, Aludo Juma Sanga (28) amefikishwa mahakama ya Wilaya ya Mbozi mbele ya Hakimu mfawidhi mwandamizi, Rahim Mushi kwa kosa la kutishia na kumdhuru Waziri wa mambo ya ndani Mheshimiwa Shamsi Vuai Nahodha.

Mwendesha mashtaka Bwana John Mazwile ameiambia mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo wakati Waziri Nahodha akiwa ndani ya gari yenye namba WMN alipokuwa katika ziara,  Februari 3 mwaka huu, majira ya saa 3 na dakika 50 asubuhi maeneo ya Mwangaza Hotel Tunduma.

Amesema kosa hilo ni kinyume cha sheria kifungu cha 89 (a) na (b), cha marekebisho ya sheria mwaka 2002 cha kanuni ya adhabu ambapo mtuhumiwa alikuwa na kipande cha mti na bendera ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

 Ameongeza kuwa mshtakiwa alizuiwa na Vijana wa ulinzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), maarufu kama Green Gurd ambapo alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Februari 6 mwaka huu.

Aidha PP Mazwile ameiambia mahakama upelelezi wa shauri hilo umekamilika na kwamba upande wa mashtaka unatarajia kuleta mashaidi wanne kwa ajili ya kutoa ushahidi na kwamba vielelezo vipo ambavyo ni kipande cha mti na bendera ya CHADEMA vilivyotumiwa na mshtakiwa huyo.

Hata hivyo kesi hiyo imeahirishwa mpaka itajapotajwa tena mwenzi April 4 mwaka huu.

Wakati huohuo Victor Mwasongole na Joyce Tenson Mwampashi wamesomewa shtaka la mauaji ambapo imedaiwa na mahakamani hapo washtakiwa kwa pamoja walimuua Dominick Richard, eneo la Ichenjezya wilaya ya Mbozi mkoani hapa.

Kosa hilo limetajwa kuwa ni kinyume cha sheria kifungu cha 196 (a) na (b) sura ya 16 cha marekebisho ya sheria ya mwaka 2002.

Katika kosa hilo watuhumiwa hawakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza na keshi hiyo itatajwa April 10 mwaka huu.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger