Pages


Home » » MAJERUHI WA TUKIO LA MAPIGANO YA CHILULUMO, WILAYA YA MBOZI MKOANI MBEYA.

MAJERUHI WA TUKIO LA MAPIGANO YA CHILULUMO, WILAYA YA MBOZI MKOANI MBEYA.

Kamanga na Matukio | 05:43 | 0 comments
 Mmoja wa wananchi waliojeruhiwa kwa kipigo kufuatia mapigano yaliyozuka katika Kijiji cha Chilulumo Wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya Bwana Daudi Sikali.
Mabinti waliodhalirishwa kijinsia baada ya kubakwa na watu saba walionadaiwa kushinikizwa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Chilulumo, Wilaya ya Mbozi, Mkoani Mbeya Bwana Bruno Chipungu, huku wakishikiwa mashoka kutenda ukatili huo wa ubakaji kwa mambinti.
*******
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Chilulumo, Wilaya ya Mbozi, Mkoani Mbeya Bwana Bruno Chipungu amefikishwa mahakamani kujibu kosa la kutishia kuua Machi 12 na 15 mwaka huu kijijini hapo.

Mtuhumiwa huyo alisomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya hiyo Rahim Mushi, ana mwendesha mashtaka mkaguzi wa Polisi (PP) John Mazwile March 21 mwaka huu.

Akisoma shtaka mwendesha mashtaka huyo amesema mtuhumiwa aliteka kosa hilo la kutishia kuua kinyume cha sheria, kifungu cha 89 sura ya 16 cha marekebisho ya sheria ya mwaka 2002.

Mwenyekiti huyo (mtuhumiwa) na uongozi wa kijiji hicho wanatuhumiwa kuwa vinara katika mgogoro kijijini hapo na kusababisha baadhi ya wananchi kujeruhiwa na mabinti watatunkubakwa, kuharibiwa mali na wengine kuchomewa nyumba zao hali iliyopelekea baadhi ya wananchi kuishi uhamishoni kwa hofu ya kuawa.

Aidha, PP Mazwile alizuia dhamana kwa mtuhumiwa na hivyo kwenda mahabusu hadi, kesi hiyo itakapotajwa tena mahakamani hapo mwenzi ujao na mpaka sasa watuhumiwa wanne wamefikishwa mahakamani hapao kutokana na vurugu zilizozuka kijijini hapo.

Wakati huohuo Jeshi la Polisi mkoani hapa, linamshikilia mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Mariam mkazi wa Mwanjelwa jijini Mbeya, baada ya kummwagia maji ya moto Joseph Simfukwe (35).

Tukio hilo limetokea Machi 21 majira ya saa 2;30 usiku ambapo, Bwana Simfukwe alikwenda kwa Mariam kufuatilia sahani zake alizokuwa akizitumia katika biashara yake ya kuuza chipsi ndipo binto alimdai deni lake la shilingi mia nne, alipomwambia atampatia baadae ndipo aligadhibika kisha kuchukua maji ya moto na kummwagia Josephat, mwilini huku akiporomosha matusi mazito huku Josephat akianguka chini chini kwa maumivu makali.

Josephat amejeruhiwa vibaya mwilini na amelazwa katika Hospitali ya  Rufaa jijini Mbeya wadi namba 1 akipatiwa matibabu.

Aidha Julius Mkela mkazi wa Ifumbo Chunya amejeruhiwa vibaya baada ya kupigwa kisha kuporwa dhahabu na pesa taslimu ambazo idadi yake haijafahamika usiku wa Machi 18 mwaka huu, ambpo majambazi walivamia nyumbani kwake na kumlewesha kwa madawa na kuanza kupekua kila eneo na kufanikiwa kuchukua dhahabu kiasi kikubwa na pesa taslimu kisha kutokomea na kumwacha Julius Mkea akiwa hajitambui.

Diwani wa Kata ya Ifumbo Michael Zanzi amethibitisha kutokea kwa tukio hili na kwamba wameripoti kituo cha Polisi na mpaka sasa Mkea amelazwa.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger