Pages


Home » » MAJAMBAZI WAWILI WAUAWA, MAHABUSU WACHIMBA UKUTA KITUO CHA POLISI KATI MBEYA KISHA KUTOROKA.

MAJAMBAZI WAWILI WAUAWA, MAHABUSU WACHIMBA UKUTA KITUO CHA POLISI KATI MBEYA KISHA KUTOROKA.

Kamanga na Matukio | 05:44 | 0 comments
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi, akiwa ameketi ofisini kwake.
 **********
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbozi.
Watu wawili wanaosadikiwa kuwa majambazi wameuawa na wananchi wenye hasira kali katika Kijiji cha Myunga, Wilaya ya Momba (Jimbo la Mbozi Magharibi) mkoani Mbeya.

Majambazi hayo yameuawa usiku wa manane yalipokwenda katika kijiji hicho kwa nia ya kutekeleza mauaji kwa diwani wa Kata ya Myunga (CHADEMA) mheshimiwa Godfrey Siame, ambapo waliahidiwa kupewa milioni mbili.

Majambazi hayo yakiwa na silaha mbili aina ya shortgan na bastola walipofika kijijini hapo na kisha kumrubuni Diwani huyo kuwa wanataka kudanya naye biashara, ndipo aliwashitukia kuwa ni majambazi wakati  yeye akiwa Tunduma baada ya mtego  wakati wakitoka katika nyumba moja ya kulala wageni kwa ajili ya kutekeleza azma yao walikamatwa na wananchi wenye hasira kali na kuanza kupingwa hadi kuuawa.

Wakati huohuo usiku wa kuamia jana mahabusu wanne waliokuwa katika mahabusu ya polisi Kituo Kikuu cha Kati Mbeya wametoroka baada ya kufanikiwa kuchimba ukuta wa vyumba vya mahabusu bila Askari waliokuwa zamu kujua.

Askari hao walifanya ukaguzi majira ya saa nane usiku saa tisa usiku wakabaini mahabusu hao hawapo baada ya kuchimba moja ya ukuta kisha kutokomea gizani na kuwaacha Polisi wakiwa katika lindo.

Mbinu iliyotumika ni kuloanisha ukuta kwa kutumia maji yaliyopo bafuni na vipande viwili vya nondo ambavyo walivitumia kuuchimba ukuta huo kwa urahisi licha ya kujengwa kwa matofari ya saruji.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa matukio yote wawili na kwamba mahabusu watatu walikuwa wanakabilisha na kesi za mauaji na mmoja kesi ya wizi.

Hata hivyo amesema Jeshi lake limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja ambaye ni Fadhili Mwaitebele (27), mkazi wa Ilomba jijini Mbeya ambaye alikuwa anatuhumiwa kwa wizi.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger